Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kwamba unalinganisha Morocco na Tanzania vivutio? Hebu kuweni serious aisee,Tanzania haiwezi kujenga kiwanja kama hicho kwa hali hii ya sasa ambapo nchi inatawaliwa na wafisadi watupu.
Nashangaa Morocco ambayo ukilinganisha na Tanzania kwa rasilimali na hata vivutio tofauti ni kama usiku na mchana lakini vitu wanavyofanya katika nchi yao Tanzania hawawezi kufanya mpaka mwisho wa dahari.
Viwanja vya Morocco kwenye Afcon iliyopita vilikuwa vyenye viwango sawa na Ulaya au Marekani viwanja ambavyo kamwe Tanzania haiwezi kuwa na ndoto ya kumiliki hata siku moja.
Labda hujanielewa, yaani Tanzania pamoja na vivutio kibao lakini kimaendeleo Morocco wanatuzidi mbali sana.Kwamba unalinganisha Morocco na Tanzania vivutio? Hebu kuweni serious aisee,
Morocco Wana vivutio zaidi yetu, ni katika Nchi yenye vivutio zaidi Africa, kuna Nchi 3 Africa ambazo zinavutia zaidi watu kutembelea, Egypt then Morocco then South Africa.Labda hujanielewa, yaani Tanzania pamoja na vivutio kibao lakini kimaendeleo Morocco wanatuzidi mbali sana.