Morogoro: Afisa anayetuhumiwa kuingia mitini na fedha za madereva za kulipia Leseni za LATRA asimamishwa kazi

Morogoro: Afisa anayetuhumiwa kuingia mitini na fedha za madereva za kulipia Leseni za LATRA asimamishwa kazi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Dar es Salaam, 18 Julai, 2024

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) iliona taarifa zilizosambaa kupitia mtandao wa Jamii Forums tarehe 17 Julai, 2024 kuwa, "Afisa anayejulikana kwa jina la Fadhili anawalazimisha Madereva wampe fedha awalipie Faini na Stika za LATRA kwa madai mfumo unasumbua."

Taarifa hiyo iliomba LATRA Mkoa wa Morogoro imchunguze Afisa huyo anayetumia Madaraka vibaya na kuwatisha Madereva Bajaji.

Mamlaka imewasiliana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, ambayo, ina Hati ya Maelewano (MoU) inayoiwezesha Halmashauri hiyo Kutoa Leseni za LATRA kwa Pikipiki za Magurudumu Mawili (Bodaboda) pamoja na Pikipiki za Magurudumu Matatu (Bajaji) na kubaini kuwa;

• "Afisa" anayetuhumiwa ni Bw. Fadhili Elieza, ambaye ni mwajiriwa wa muda mfupi (temporary staff) katika Halmashauri hiyo idara ya ukusanyaji wa mapato; na Kufuatia tuhuma hizo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, amemsimamisha kazi Bw. Fadhili Elieza ili kupisha uchunguzi, na mtuhumiwa atachukuliwa hatua stahiki endapo atabainika kutenda kosa.

Aidha, LATRA imewasiliana na Bw. Omary M. Mpulila, Katibu wa Umoja wa Wamiliki wa Bajaji Mkoa wa Morogoro ambaye amesema kuwa umoja huo haujawahi kupokea malalamiko ya wanachama wake kutishwa au kuombwa rushwa wanapohitaji leseni za LATRA. Taarifa hizo zinapaswa kuchunguzwa kwa umakini zisiichafue LATRA inavyoboresha huduma zake kwa wateja kwa uwazi na bila vishawishi vya rushwa.

Mamlaka inakemea vikali vitendo vyote vya rushwa katika utoaji wa huduma zake, na inatoa wito kwa wadau wake na wananchi wote kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kupitia namba 0800110019/20 bila malipo, zinazofanya kazi siku zote (24/7).

Salum Pazzy
MKUU WA KITENGO CHA UHUSIANO NA MAWASILIANO
LATRA Makao Makuu, S. L. P. 1742, 41104 Tambukareli, Dodoma

IMG_20240718_221004_490.jpg
 
Back
Top Bottom