Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Wakazi wa Morogoro, hasa tunaoishi maeneo ya Kihonda na Manyuki, tunakabiliwa na changamoto kubwa ya barabara, hususan kipindi cha mvua. Barabara ya Manyuki inayotokea Mazimbu imeharibika, na sehemu nyingi zilizofanyiwa makarabati zimeanza kuharibika tena.
Aidha, maeneo mengi ya barabara hiyo hayana mitaro rafiki ya kupitisha maji jambo ambalo limeongeza kero maji kujaa kwenye maeneo ya barabara.
Kutokana na hali hiyo, mvua zinaponyesha barabara inakuwa haipitiki hadi magari yanakatiza ruti. Vilevile, nyumba nyingi huathirika na mafuriko hata pale zinaponyesha mvua ndogo ndogo.
Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba makalavati mengi yameanza kumeguka kwa muda mrefu bila kufanyiwa marekebisho yoyote. Hali hii inasababisha barabara kuendelea kumomonyoka, jambo ambalo linaweza kuwa hatari zaidi siku zijazo kutokana na maji kukosa mwelekeo.
Natoa wito kwa mamlaka husika kuboresha miundombinu ya barabara hiyo, ikiwemo kuboresha mifumo ya kupitisha maji kama vile makalavati na mitaro. Pia ni vyema itengewe bajeti kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami, kwani ina mashimo katika maeneo mengi, hali inayochangia kuharibika kwa vyombo vya moto.