Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Wadau mada inajieleza; nimeshitushwa sana nimepita Morogoro eneo la Mkundi ambako mwaka jana tu miezi ya mwishoni ulifanyika ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua kandokando ya Highway ya Morogoro - Dodoma. Mvua iliyonyesha siku chache zilizopita imesomba mawe yote yaliyojengwa kwa cement na mchanga na kuiacha mitaro wazi kabisa. Kiukweli ile ni hujuma na ubadhirifu wa wazi kabisa uliofanywa na Mamlaka zilizopewa dhamana ya kusimamia fedha za kodi zetu.
Kumradhi nimeshindwa kupiga picha kwakuwa nilikuwa kwenye usafiri wa public, naamini wapo wana-Morogoro humu walioona ubadhirifu huo wanaweza kutusaidia kupost picha humu kama kielelezo.
Angalizo:
Habari hii haijalenga kumchafua mtu, nimeileta hapa ili wahusika wajitathimini kama kweli wanaitendea haki fedha ya kodi tunayolipa. Waandishi wa habari mnaweza kusaidia kuifikishia taarifa serikali kuu, kwakweli inasikitisha, inahuzunisha na kuumiza sana.
Nawasilisha