Nimekuelewa ila utambue tu nchi hata kama mimi na wewe tutafanya kazi vipi our efforts zitaishia kubadili familia zetu na vizazi na hiyo sio issue ya msingi..Hapa tunaongelea taifa...serikali inayoweka sera za elimu, urban planning policies, inayotengeneza sera, sheria na kuzisimamia..ndio maana nikatolea mfano wa hizo nchi.
Zote hizo zimebadilishwa na watu (extra ordinary smart people) waliokuja na solutions za kutoa nchi zao kwenye umasikini. Just pick one nenda kasome Singapore ilikuwa nchi ya aina gani na nani aliyeleta mabadiliko ya kiuchumi.
Hauwezi tegemea mabadiliko kwenye taifa unapeleka darasa la 7 bungeni. Sahau.
Nimekuelewa pia, lakini never underestimate the power of individual initiative, the power of bottom up approach katika kuleta mabadiliko.
Mfano kidogo, kuhusu nyumba na makazi.
Ukitembelea miji karibu yote ya Tanzania kuna mabati ya msauzi yapo kwenye fashion, na kuna ile design ya paa inayoinuliwa hadi mbinguni.
Unadhani zile style na design zimelazimishiwa kutoka juu? No. Ni watu wameanzisha na wengine wameigana na voila! tuna linchi limejaa nyumba za style moja.
Mfano mwingine. Usafi wa miji na mitaa, kutotupa taka kiholela. Magufuli kaja na style ya kusafisha mazingira kwa mikono yake mwenyewe ili awainspire raia anaowaongoza hadi ikawekwa siku moja kila mwezi ya kusafisha mazingira. Ah wapi! Nenda hata kesho mijini ucheki watu wanakula miwa, machungwa, mahindi na kutupa popote maganda. Top down approach doesn't seem to work as efficiently as needed kwa nchi yetu.
Suala la mipango miji ni konki zaidi. Pale jangwani ilikuwa kila mwaka mafuriko yanasomba nyumba kadhaa, serikali inafanya sehemu yake lakini ah wapi, mvua zikitulia watu wanarudi pale pale.
Mtu kama hajakomboka kiakili nchi itapiga mark time muda mrefu sana hata huko mbeleni. Na nafikiri kuna tofauti sana kati ya maeneo makongwe ya miji (wanakokaa wazawa wa asili wa maeneo yale) na maeneo mapya ya miji (ambako walikuta viwanja vilishapimwa).
Mambo mengine yanayofanya miji yetu isionekane imepangwa ni mfumo wetu wa umiliki ardhi. Nchi yetu ina historia ya ujamaa kwamba hata maskini anaweza kumiliki ardhi na kujijengea anavyotaka na anavyoweza. Ulaya na kwingineko ardhi ni mali ya makabaila wachache wanaojenga na kuwauzia au kuwakodisha wengine. Kama tunataka hadi Magomeni pawe kama Masaki na Oysterbay tukubali tu kuwaachia real estate tycoons wapaendeleze kama wawekezaji kwenye real estates. Tutakubali?