Morogoro: Meneja wa MORUWASA asimamishwa kazi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amemsimamisha kazi, Meneja wa usambazaji maji Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) Eng Thomas Ngulika kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Waziri Aweso ametangaza uamuazi huo leo Jumanne tarehe 23 Julai 2024 akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Morogoro.

"Hatutokuwa tayari kuona mtu kwa maksudi anatoa taarifa za uongo, wakati yeye ndiye anayehusika katika hilo jambo, eneo la Tungi, nane nane na maeneo mengine wiki tatu hawakupata maji, namuuliza Mtendaji anaongea uongo wewe unamwambia moja mbili tatu karekebishe, anarekebisha leo watu wanapata maji" amesema Waziri Aweso na kuongeza

"Huyu mtu wetu ambaye anahusika na suala la Technical atatupisha, bodi ipo hapa mumsimamishe mara moja la pili acha mimi niende kwenye kikao ipo timu yangu hapa inanifanyia kazi nitawasaidia lakini lazima twende" ameeleza.

Pia Soma:
~ MORUWASA: Tuna upungufu wa uzalishaji maji kwa 49% ndio maana Morogoro kuna mgao
~ Waziri Aweso unasema DAWASA kuna hujuma? Njoo Morogoro, huduma ya Maji ni kero kubwa
 
Mkoa wa Morogoro umebarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya maji lakini cha kushangaza Kuna maeneo mengi katikati ya mji hayapati maji kabisa mengine yanapata mara moja Tu kwa week.
 
One love Tz🇹🇿🇹🇿🇹🇿
Umoja wetu kwa maendeleo ya Taifa. Wazembe hawatufai.
 
Morogoro ina mito kibao ila maji hamna mfano mzuri tyu ni njia ya kwenda ifakara pale madaraja 12
 
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amemsimamisha kazi, Meneja wa usambazaji maji Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) Eng Thomas Ngulika kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Waziri Aweso ametangaza uamuazi huo leo Jumanne tarehe 23 Julai 2024 akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Morogoro.

"Hatutokuwa tayari kuona mtu kwa maksudi anatoa taarifa za uongo, wakati yeye ndiye anayehusika katika hilo jambo, eneo la Tungi, nane nane na maeneo mengine wiki tatu hawakupata maji, namuuliza Mtendaji anaongea uongo wewe unamwambia moja mbili tatu karekebishe, anarekebisha leo watu wanapata maji" amesema Waziri Aweso na kuongeza

"Huyu mtu wetu ambaye anahusika na suala la Technical atatupisha, bodi ipo hapa mumsimamishe mara moja la pili acha mimi niende kwenye kikao ipo timu yangu hapa inanifanyia kazi nitawasaidia lakini lazima twende" ameeleza.

Chanzo: East Africa TV
Hongera Mhe. Waziri Aweso kwa maamuzi magumu, hii nchi inahitaji mabadiliko.
 
Watumishi wengi sio wote wa Umma hasa Viongozi wanafanya kazi kwa mazoea, pia ni wabinafsi.
 
Back
Top Bottom