Morogoro: Msanii Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego', akamatwa na Polisi

Morogoro: Msanii Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego', akamatwa na Polisi

Atashughulikiwa vilivyo kwa kosa la kutoa maoni yake! Hii ndo nchi yetu kwa sasa. Muda si mrefu itakuwa tofauti!
Uhuru gani mnautaka watanzania? Wa kutukana viongozi jinsi mnavyotaka, sio kwa serikali ya magu, mtaisoma namba
 
Ni kweli au ni uzushi kama ilivyo habari nyingine nyingi.
 
sababu nini??
Kufanya kazi ya Fasihi BILA KUTUMIA Fasihi. Waimbaji wanafikiri kuwa USANII ni uhuni na kukusanya maneno na midundo. Fasihi ni MATUMIZI ya LUGHA katika namna ya ufundi kuelimisha, kuburudisha na kufikisha UJUMBE KI-SANAA......
 
Yesu alimaliza kazi yake ndipo akasurubiwa lakini mbegu ya neno ilikuwa ishapandwa kwenye mioyo ya wanadamu..

Ney kasha fanya kazi...
Kumkamata nikusaidia tu wimbo uwafikie watu wengi zaidi,wengi watataka kujua ameimbaje hata kumpelekea akamatwe?; kwa hivyo serkali inajitshidi kujinyoga yenyewe
Kaimba kipi kipya ambacho hatujakisikia? C upuuzi tu, wacha akanyee debe
 
Baraza la sanaa la taifa ndilo linawajibu wa kushughulika na kazi za sanaa na wasanii ikiwemo content ya kazi zao

Msanii akitoa kazi inayokuwa na content isiyo na maadili au isiyokubalika na jamii ya watanzani, ni BASATA ndio wanatakiwa kushughulika na msanii husika hata kumpatia adhabu inayostahili ikiwepo kuifungia kazi husika na msanii mwenyewe

hii ni tofauti kwa Nay wa Mitego!
kwa nini Amekamatwa na polisi ilhali BASATA ipo?
hapa jeshi limeingilia majukumu ya Basata!
ni nani katoa order ya Nay kukamatwa bila ya Basata?
 
Respect ipi anayotafuta Magu??Ya kutukana waliompigia Kura??

Hivi unawaambia RAIA wako wanapenda Umbea wakati Kiongozi unasikiliza kipindi cha Shilawadu??

Kama wanapenda Respect afuate sheria.Ukiona hivyo ujue watu wamechoka.Ndiyo ajifunze kutumia kauli njema na pia aende haki.

Kwani kuna MTU anaitwa Bashite??
Uhuru mnaoutaka not to that extent ya kutukana hovyo serikali bila kuwa na hoja zenye mashiko, wacha magu afanye kazi yake
 
Back
Top Bottom