Morogoro: Msanii Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego', akamatwa na Polisi

Morogoro: Msanii Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego', akamatwa na Polisi

Ney anajionaga yeye ndio mtabe wa Tz nzima. Nyimbo zake nyingi huwa za hivyo hovyo. Kwa wimbo wake huu kavuka mipaka. Heshima Hakuna kabisa. Ebu afundishe adabu kwanza.
 
Nchi ya jasho machozi na damu

Hakuna namna inabidi tumpende kwa nyuso zetu kukubari anachotaka wakati mioyo yetu ikiwa haimtaki na kumsahau kuwa hatuna rais kama huyu.
 
Mi najiuliza. Hivi akifikishwa mahkamani. Mlalamikaji ni nani?
 
Weshaona fashion sikuizi kutukana, wameharibu jf sikuhizi nayo hovyo tu, huyo wanayemuiga yuko States na hawezi kanyaga Tz, muda si mrefu jf tunaipoteza maana naona hata mods ni kama wanatumika.
we ndo ney wa mitego? alafu ney hajatukana katoa hisia zake. kama kuna mtu anahisi ametukanwa si aende mahakamani.

mi ninavyojua hakujawahi kuwa na daudi mwenye vyeti feki huko kolomije. kwa hiyo ney katumia wahusika hewa.

pili nchi aliyoitaja ney sio tanzania kwa kuwa tz tuna raisi anayeshaurika. anayejiamini mkweli. ncho ambayo ina uhuru wa kuongea.

hakuna kesi ya kujibu hapo labda kumkomoa asipate dhamana asote maaabusu. kesi ikifika mahakamani inakufa
 
Katika hiyo mistari hakuna cha kumtia hatiani..

Kwanza hajataja jina la nchi..

Pili,hajataja jina la huyo dokta wa kutumbua majipu,au kuna mtu ni dokta wa kutumbua majipu??

Tatu,huyo kichaa aliyepewa rungu hajatajwa kwa jina lake..kwahiyo yaweza kuwa hata ni kichaa mmoja wa huko mvomero..

Nne, Bashite ni nani? Hawawezi kujiingiza katika huo mtego maana watakuwa wamepigia mstari na kuzihalalisha tuhuma zote!
 
Yaani ni kama lissu alipowaaambia mleteni huyo dikteta uchwara ajibu kuwa nimemtukana. Na ney ataomba huyu mtu ambaye hataki ushauri aje aseme kweli yeye ndi ndugu yake na Yesu??
 
Msanii wa kizazi kipya Emanuel Elibarik alimaarufu kama NEY wa mitego amekamatwa asubuhi hii huko morogoro

View attachment 486993



Sehemu ya wimbo wa Ney wa Mitego:

=======

Hivi Uhuru wa Kuongea bado upo? Siamini nchi inaendeshwa kwa kiki!
Nasikia kuna viongozi wamefoji vyeti? Wapooo! Mheshimiwa hivi unamjua Bashite kutoka Kolomije? We si Dokta wa kutumbua majipu?

We mtu gani sasa? Hutaki kushauriwa, hutaki kukosolewa? ...Naona kichaa kapewa rungu! Hahahaha

Sasa hapa tusi liko wapi hii nchi siyo monarchy hadi mkuu asikosolewe hata wakienda kwa cort lazima wabwage maana hapo wanahisia tu kuwa fulani kasemwa. Na lissu atanunua hiyo kesi. Nchi za wenzetu wale marepa wa marekani na mabobu wote walizisema serikali zao mpaka zikanyooka.
Usione leo mnakimbilia kuishi marekani na ulaya kuna watu sampuli ya akina ney wa mitego, lema, lissu walisota.
Acheni kushabikia ujinga wa serikali yetu kutokuwa double standard kwa haki.
Bashite tunataka vyeti vyako tafadhali.
 
We mtu gani sasa hutaki kushauriwa,hutaki kukosolewa,
Umelogwa wewe unajiona ndugu yake na yesu eeeeh

[emoji1] [emoji1] [emoji115] [emoji115] [emoji115] [emoji1]

Kwa voice ya Nay wa mitego


Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
Apae Mbinguni basi kama yeye nisawa na Yesu. Rais gan hana utu.!
 
Nilipousikia huo wimbo tu nikajua jamaa lazima akamatwe. Ile lugha aliyotumia ni kali sana. angejaribu kuipunguza ujumbe ungemfikia tu.

Ila kwa kuwa kataka mwenyewe, labda na yeye alikuwa anataka kiki basi lazimu imgharimu.
 
Amemkaahifu amemwambia nini???Wataisoma.number au hashauriki??Amesema.mwenyewe hashauriki.sasa!Amemtaja jina??Akili zetu wakati mwingine ni za ajabu sana.Siye tunaisikiliza ipo You tube.
Mkuu kuzaliwa na kukulia uswahilini ni shida lakini pia ukiamua kufanya vitu kwa magumashi lazima kila wakati ujishuku,yaani hata ukikuta jamaa wamekaa somewhere unahisi wanakujadiri wewe.no way unaweza kuishi kwa amani ukiwa unafanya vitu vya hovyo kwa jamii
 
Back
Top Bottom