Inajulika miaka mingi mvua zikianza kunyesha ukanda wa Morogoro kwa wingi wanaodhurika na maji ya mvua hizo ni wakazi wa wilaya za Liwale na Kilwa, mkoani Lindi.
Kuna wakati mvua zinasababisha barabra kuu ya Mtwara-Dar kufungwa kutokana na kukatika kwa madaraja eneo la Somanga. Sasa kwa mvua zilizoanza Morogoro ambazo maji yake huwa yanaelekea Kilwa kama mtu huna safari ya ulazima kwenda mikoa ya Lindi na Mtwara tulia kwa sababu ujenzi wa madaraja Somanga toka mwaka jana hadi leo haujakamilika. Vinginevyo uwe tayari kuzungukia Songea au upande ndege.
Mbali na athari kwa wasafiri kuna wananchi wamejenga kando ya mkondo wa daraja la Mkapa na mamlaka zimekaa tu zimetulia wanangoja watu wafe wanasiasa wakapate cha kuongea. Maeneo ya Somanga, Tigi, Nyamwage na Muhoro yale sio makazi ya binadamu. Hata isiponyesha mvua kubwa ya kusababisha barabara kuu ya Dar- Mtwara kufungwa nyumba za wakazi wa maeneo hayo zinakuwa zimezingirwa na maji hadi huruma.