Nina frame mjini Morogoro, eneo la Sabasaba, eneo zuri kabisa kwa biashara ya nguo (nafuu), viatu, jezi, nk, jumla na rejareja. Pia ni eneo lenye mnada siku ya Jumapili.
Tatizo sina mtaji wa kutosha kama wanaonizunguka… nakuita wewe mwenye mali, njoo tushirikiane, lete mali tuuze, upate chako, nipate changu kadri ya makubaliano.
Kuna wakati niliwahi kupitia changamoto kama hii ya kwako! Uamuzi niliouchukua ulikuwa ni ule wa kubinafsisha tu ile frame kwa mtu mwenye mtaji, na aliyejipanga. Na wala sikuwahi kuwazia habari ya ushirika.