The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Julai 8, 2021 anashiriki Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku Mbili Mkoani Morogoro.
Updates:
Salamu za wanawake wa CCT
i) Ukatili kwa kijinsia
Tunakushukuru kwa jitihada na harakati zote zinazoendelea katika kupunguza tatizo la ukatili wa kijinsia. Hata hivyo, uwepo wa vitendo vya ukatili umeendelea kujitokeza katika jamii.
Sisi wanawake wa CCT tunaomba mabadiliko yafanyike katika mfumo wa jinai ili kuwezesha kumalizika kwa kesi hizi kwa haraka.
ii) Vifo vya mama na mtoto
Mh. Rais, pamoja na jitihada zote zilizofanyika kupunguza vifo vya mama na mtoto, bado kuna ongezeko la vifo hivyo. Tunapendekeza kuimarishwa kwa elimu ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango unaotoa fursa kwa mama kupumzika na kuwa na afya na uzazi salama na kupunguza matatizo ya udumavu wa Watoto.
iii) Mimba na ndoa za utotoni
Kuna viashiria vya ongezeko la mimba na ndoa za utotoni, tatizo linalofanya watoto wa kike kushindwa kuendelea na masomo na kushindwa kutimiza ndoto zao.
Tunaomba mabadiliko ya Kisera, Kisheria na Utaratibu ambazo zitawezesha Watoto wa kike kurudi kwenye mfumo rasmi wa elimu.
iv) Nafasi za ajira na uongozi kwa wanawake
Mh. Rais, tunakupongeza kwa kutambua na kuongeza fursa za wanawake katika nafasi za uongozi. Sambamba na hilo, yunaomba uelekeze nguvu zaidi kwa nafasi za ajira kwa wanawake katika Nyanja mbalimbali.
Rais Samia Suluhu Hassan
Dini zetu zina mchango mkubwa sana katika kuweka amani, utulivu lakini pia na maadili katika mataifa yetu.
Nawapongeza kwa kutoa huduma mbalimbali za kijamii kwa Watanzania. Huduma ya usaidizi wa kisheria, elimu pamoja na afya.
i) Changamoto ya ugumu wa kupata 'work permit'
Baba Askofu Cheyo ametaja changamoto mbalimbali zinazowapa ugumu katika kutoa huduma. Ametaja changamoto ya kupata vibali vya kazi (work permit) pamoja na vibali vya kuishi (resident’s permit) kwa wataalamu wa kujitolea kutoka nje katika taasisi zenu za elimu na afya.
Mtakumbuka, wakati nawaapisha makatinu wakuu, mimi pia nilieleza suala hili kwa kirefu. Nashukuru Idara ya Uhamiaji na Idara ya Kazi wamelifanyia kazi suala hili ambapo tangia tarehe 23 Aprili mwaka huu wa 2021 wameanzisha mfumo wa kielektroniki (online work permit issuance system) ambapo umepunguza sana urasimu. Nimeambiwa hivi karibuni kuwa kama muombaji atakuwa amekamilisha taratibu zote, atapata vibali hivyo ndani ya siku 1 hadi 3 kutoka siku 14 au zaidi.
Nilisisitiza kuondoshwa mfumo huu ili kuondoa kuonana kwa mtu una mtu. Inaondosha kuzungushana na mazingira ya rushwa.
ii) Kodi kwa taasisi za kidini
Baba Askofu Cheyo pia amezungumzia suala la kodi kwa taasisi za kidini zinazotoa huduma za afya na elimu. Niliambia suala hili nilipokutana na TEC, nina hakika nikienda BAKWATA nitakutana nalo pia.
Tunalazimika kutoza kodi kwa taasisi za elimu na afya za kidini kwasababu baadhi ya taasisi hizo zina mazingira ya kufanya shughuli hizo kibiashara na siyo kihuduma.
Hapa ndipo panapokuja lile suala linalolalamikiwa la ushindani wa huduma, taasisi ya dini ina hospitali yake hapo Serikali inajenga kituo cha afya hapo kwa kuona wananchi wakienda huku wanatoa pesa nyingi zaidi kuliko wakipata huduma serikalini.
Pia inafanya Serikali kufanya vitu mara mbilimbili kwa kuweka huduma ileile inayopatikana kwa kuweka sehemu moja ambayo sio mtindo mzuri
Lengo la serikali ni kupunguza ugumu wa maisha.
Suluhusho la hili ni tufanye kazi kwa uwazi na kuaminiana ili watoza kodi wajue taasisi za dini hazifanyi biashara, ni lazima mahesabu yawe wazi.
Ni kweli kumetokea shida mbili-tatu katika mifumo hiyo. Kuna shule ambazo zinatoa huduma; zinapata msaada kutoka nje – elinu au afya – lakini bado taasisi zetu za kodi zimekwenda kuwatoza. Ukilitizama unaona hakuna mantiki. Hiyo yote ni kwakuwa hakukuwa na uwazi. Niombe sasa tufanye kazi kwa uwazi na kuaminiana.
Ukiangalia rates za taasisi binafsi na za dini zinazotoa huduma hizi, zinafanana. Hii ndiyo sababu ikaonekana kuwa taasisi za dini pia zinafanya biashara.
Tukiondoa kodi kwa taasisi za kidini ambazo utendaji wake ni sawa na ule wa taasisi za sekta binafsi, hakutakuwa na level battle field. Sekta binafsi watashindwa kufanya biashara.
Serikali imeanza kufanya mapitio ya kodi na kufuta kodi kadhaa. Katika hilo nitoe taarifa kwamba katika Kodi ya Fedha ya Mwaka 2021\22 imefuta tozo ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (SDL) ambayo ilikuwa ninalalamikiwa siku nyingi na hospitali za taasisi za dini. Kwahiyo, tumefuta tozo hiyo lakini kwa ujumla, tunaenda kuangalia mfumo wote wa kodi ya nchi yetu.
iii) Ushirikiano na taasisi binafsi, dini
Pia, Maaskofu niwahakikishie kuwa Serikali imekuwa na ushirikiano wa dhati kabisa na sekta binafsi kujenga mazingira bora ya biashara na kukuza utendaji na ufanisi wa sekta hiyo.
Tunapomba viongozi wa dini mutoe taarifa hizi za maradhi ya Covid-19, tunaomba mtoe taarifa wapate maarifa ili wajikinge, wasiangamie. Tunapoomba mtusaidie kuelimisha kuhusu sensa itakayokuja mwakani, ni kutoa maarifa kwa watu wajue umuhimu wa sensa na wakubali kuhesabiwa.
August mwakani tutakuwa na Sensa ili tujue idadi yetu tuko wangapi, takwimu za idadi ya Watu zinaisaidia Serikali bila takwimu mipango ya maendeleo ni kama mnabahatisha tu, niwasihi Vingozi wa Dini kuwahimiza Wananchi kuachana na imani potofu na kushiriki zoezi hili
Tunapoomba mtoe taarifa za elimu ya uraia, ni kupeleka maarifa kwa watu wapate maarifa ili wakae mstari ulionyooka.
iv) Kuheshimu Utawala Bora
Naahidi serikali itaendelea kuheshimu misingi ya utawala wa Utawala wa Sheria na Haki za Binadamu na hatutosita kuchukuwa hatua dhidi ya Viongozi au watendaji wa Serikali wasioheshimu Utawala Bora na kukiuka Haki za Binadamu.