Morogoro Rd: Kibanda Cha Mkaa - Wananchi wamefunga Barabara muda huu! Mbezi hakuendeki

Morogoro Rd: Kibanda Cha Mkaa - Wananchi wamefunga Barabara muda huu! Mbezi hakuendeki

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,203
Reaction score
37,906
Morogoro Rd: Kibanda Cha Mkaa - Wananchi wamefunga Barabara muda huu! Mbezi hakuendeki

Wananchi wanasema watoto wanagongwa sana na Magari mahali hapa japo kuna ZEBRA.

Ushauri wangu wale mnaoelekea MBZ au Kibaha, tafuteni Njia mbadala!

20230329_170645-jpg.2570099

20230329_170638-jpg.2570101
 
Hiyo barabara ndipo napopita kila siku ukweli hapo siyo sehemu salama ya kuvuka hata kwa watu wazima.

Madereva wanakimbizana hovyo hawafuati sheria sijui ni kwa sababu pana kona labda zebra huwa hawaioni?lakini kutoka ilipo hiyo kona na ilipo zebra crossing ni kiasi cha metre 30 kwa umbali huo unaweza kuona jinsi watu wasivyotii sheria.
 
Police wako wapi, hao wananchi nao wanakosea sana, highway huwezi weka matuta, sbb utaua watu wengi sana ukiweka matuta..

Hao watoto inatakiwa traffic light ndio wapite, sio kila mahala wanapita, highway ukiweka matuta kila siku ni ajali tena mbaya sana na vifo vingi, hao, wananchi wao wanajua matuta tu, polisi wawakamate haraka
 
Zebra ya kibanda cha na zebra zote za hiyo highway zimekaa kimchongo sana,solution ya maengeneer hapo itakua ni kuweka matuta kwenye highway badala ya daraja la wavuka kwa miguu 😃
Then hakuna haja ya kuiita highway kama unajaza matuta,hao walikosea toka mwanzo wangeweka chamber za kuvukia chini.

Mbezi mwisho kutoka shell zamani wamejaza mavyuma sasa sijui kwa akili zao walitegemea kuweka barabara nzima!
 
Hiyo barabara ndipo napopita kila siku ukweli hapo siyo sehemu salama ya kuvuka hata kwa watu wazima.

Madereva wanakimbizana hovyo hawafuati sheria sijui ni kwa sababu pana kona labda zebra huwa hawaioni?lakini kutoka ilipo hiyo kona na ilipo zebra crossing ni kiasi cha metre 30 kwa umbali huo unaweza kuona jinsi watu wasivyotii sheria.
Ile barabara ukivuka taa za kwa msuguli inatamanisha kukimbia,pale kibanda ile zebra ipo kwenye bus stop ya mchongo,madereva wasio makini awi na tahadhari kama bus liliposimama kushusha abiria mbele kuna zebra,shida inaanzia hapo,kwa sasa ile zebra wangeitoa pale karibu na kituo
 
Ile barabara ukivuka taa za kwa msuguli inatamanisha kukimbia,pale kibanda ile zebra ipo kwenye bua stop ya mchongo,madereva wasio makini awi na tahadhari kama bus liliposimama kushusha abiria mbele kuna zebra,shida inaanzia hapo,kwa sasa ile zebra wangeitoa pale karibu na kituo
Upo sahihi sana.

Kwa hiyo hii inayoshikamana na stand wangeiuwa ikatumika ile kule chini karibu na daraja,natamani wahusika wangekuwa wanapita hapa waone hili wazo.
 
Barabara ni kama zinajengwa ili magari yapite
Sehemu sahihi za watembea kwa miguu ni kama suala lisilowekewa maanani kabisa unapita sehemu kuna mteremko unakutana na zebra 😃
 
Hapo ni daraja la juu Kama la manzese la wavuka kwa miguu
Mdaraja wa manzese mkubwa wote ni la kizamani,wenzetu siku hizi wanajenga simple tu au hata kuna vivuko vya underground tena huko wanaweka frem za biashara kabisa,mipango ya zebra kwenye highway walishayaacha kitambo sana
 
Police wako wapi, hao wananchi nao wanakosea sana, highway huwezi weka matuta, sbb utaua watu wengi sana ukiweka matuta..

Hao watoto inatakiwa traffic light ndio wapite, sio kila mahala wanapita, highway ukiweka matuta kila siku ni ajali tena mbaya sana na vifo vingi, hao, wananchi wao wanajua matuta tu, polisi wawakamate haraka
Unawajua madereva wa bongo na bidaboda akili zao, hata kukiwa na Taa kama hamna askari watapita tuu, dawa ni boonge la tuta
 
Then hakuna haja ya kuiita highway kama unajaza matuta,hao walikosea toka mwanzo wangeweka chamber za kuvukia chini.

Mbezi mwisho kutoka shell zamani wamejaza mavyuma sasa sijui kwa akili zao walitegemea kuweka barabara nzima!
Mkuu wewe umetembea!!!
Barabara hiii ikipoanza kujengwa niliamini ingekuwa na chamber za kuvuka chini kwa ajili ya watu hata magari yanayokatisha, kuanzia stpo over hadi kibaha. Badala yake wakaamua kuweka trafic lights ambazo ufanisi wake ni very limited.
Nchi hii wasomi wetu, wengi ni bogus , nadhani sababu ya kukariri. They'll never go out of the box . Imagine Tanroads qualification ya chini kuajiriwa ni degree!!!
 
Back
Top Bottom