Morogoro: RTO Tafadhali Shughulikia Trela Lililotelekezwa Mbugani Mikumi Bila Alama Zozote za Tahadhari

Morogoro: RTO Tafadhali Shughulikia Trela Lililotelekezwa Mbugani Mikumi Bila Alama Zozote za Tahadhari

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
Napenda kumtaarifu RTO wa Morogoro kuwa kuna trela la semi limetelekezwa tangu Jumamosi last week mpaka jana usiku mbugani mikumi kama kilomita 15 kutoka mjini, trela hilo halina alama zozote za tahadhari, halina reflective stickers wala triangle, tumepita hapo jana majira ya saa 2 na bus nusura tujigonge as mbele yetu kulikuwa na lori linakuja taa zikiwa full light

Yawezekana tukawa wachache kati ya wengi walionusurika kujibamiza kwenye hilo trela

Nawasilisha
 
Tumepita usiku ilikuwa giza na ghafla chuma hiki hapa

Wewe umesema tangia last wiki jumamosi liko hapo, umeshindwa vipi kupiga picha kama tangia juzi liko hapo.
 
Wewe umesema tangia last wiki jumamosi liko hapo, umeshindwa vipi kupiga picha kama tangia juzi liko hapo.
Nimepita Jumamosi jioni kwenda Mbeya lilikuwepo, jana nimerudi Dar usiku lilikuwepo, mimi siishi hapo lilipo, tambua nilikuwa kwenye public transport
 
Mngefanikiwa soma plate number ingesaidia hata kufanya tracing ya umiliki
 
Mngefanikiwa soma plate number ingesaidia hata kufanya tracing ya umiliki
Mkuu bora ingekuwepo hiyo number plate ingesaidia hata kuliona toka mbali, inaonekana walijua kitakachofuata waliinyofoa haipo
 
Mikumi kuna walinzi wa asili pale.
Ingekuwa sehemu ya kawaida wangeiba matairi
 
mwaka fulani ivi nakumbuka kulikuwa na wanamuziki walogongaga lori lililokuwa limesimama maeneo ya mikumi na wengi waliangamia

Hao walikuwa wanamuziki wa bendi ya Taarabu Five stars waliokufa katika ajali ya Gari Mikumi wakitoka kutumbuiza na wakiwahi Kuja Kutumbuiza Dar na waliokufa ni Issa Kijoti, Nasoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashim, Tizo ,Omari Tall, Ngeleza Hasan, Hamisa Omari, Maimuna , Haji Msanii na mcheza show wa kundi la Kitu Tigo Ilala. Na wengine wengi.
KITU TIGO enzi hizo😥
 
Back
Top Bottom