baro
JF-Expert Member
- May 12, 2014
- 3,129
- 4,028
Mh. Msajiri wa Mahakama kuu ya Morogoro, napenda kukutaarifu kuwa katika mahakama ya Mwanzo Nunge kuna Rushwa iliyokithiri.
Mahakimu wengi hapo ni changamoto sana kwa wananchi ambao ni wateja wa Mahakama wasio na uwezo wa kifedha. Mfano Kuna kesi moja ya Mirathi ambayo ni ya Mzee fulani (jina kapuni) amekuwa akizungushwa kuhusu haki yake na kupelekea kuambiwa atoe Tsh. 500,000 ili aweze kumsaidia.
Siyo huyo Mzee tu kiufupi ni kwamba rushwa imekuwa kubwa sana Mahakama ya Mwanzo Nunge na haki za wananchi wasio kuwa na pesa kuporwa na kinachofanywa ni kupindisha uamuzi wa kesi mbalimbali.
Sisi, kama whistleblowers tunaomba Msajiri wa Mahakama kuu Morogoro tupia jicho kesi zote kutoka mahakama hiyo, inaharibu image ya Mahakama.
Ili kujihakikishia mahakama fanyeni uchunguzi kwa kushirikiana na TAKUKURU, mtagundua mengi na mtakuwa mmesaidia kuokoa haki za watu zinazoporwa kwa rushwa mahakamani hapo.