DOKEZO Morogoro: TAKUKURU chunguzeni Mahakama ya Mwanzo Nunge, kunanuka Rushwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mh. Msajiri wa Mahakama kuu ya Morogoro, napenda kukutaarifu kuwa katika mahakama ya Mwanzo Nunge kuna Rushwa iliyokithiri.

Mahakimu wengi hapo ni changamoto sana kwa wananchi ambao ni wateja wa Mahakama wasio na uwezo wa kifedha. Mfano Kuna kesi moja ya Mirathi ambayo ni ya Mzee fulani (jina kapuni) amekuwa akizungushwa kuhusu haki yake na kupelekea kuambiwa atoe Tsh. 500,000 ili aweze kumsaidia.

Siyo huyo Mzee tu kiufupi ni kwamba rushwa imekuwa kubwa sana Mahakama ya Mwanzo Nunge na haki za wananchi wasio kuwa na pesa kuporwa na kinachofanywa ni kupindisha uamuzi wa kesi mbalimbali.

Sisi, kama whistleblowers tunaomba Msajiri wa Mahakama kuu Morogoro tupia jicho kesi zote kutoka mahakama hiyo, inaharibu image ya Mahakama.

Ili kujihakikishia mahakama fanyeni uchunguzi kwa kushirikiana na TAKUKURU, mtagundua mengi na mtakuwa mmesaidia kuokoa haki za watu zinazoporwa kwa rushwa mahakamani hapo.
Mahakama zote ni rushwa tupu hakuna haki
 
Mahakama za Tanzania rushwa ni kama damu kwenye mwili wa binadamu
Nakumbuka kuna mwanafunzi alikuwa anafanya mafunzo kwa vitendo mahakamani kwa siku alikuwa hakosi 20, 30 au 50 huyu alikuwa mwanafunzi je? Hakimu alikuwa anapata ngapi

Kuna na takukuru kazi yao kubwa kupalilia na kupamba rushwa
 
Mh. Msajiri wa Mahakama kuu ya Morogoro, napenda kukutaarifu kuwa katika mahakama ya Mwanzo Nunge kuna Rushwa iliyokithiri.

Mahakimu wengi hapo ni changamoto sana kwa wananchi ambao ni wateja wa Mahakama wasio na uwezo wa kifedha. Mfano Kuna kesi moja ya Mirathi ambayo ni ya Mzee fulani (jina kapuni) amekuwa akizungushwa kuhusu haki yake na kupelekea kuambiwa atoe Tsh. 500,000 ili aweze kumsaidia.

Siyo huyo Mzee tu kiufupi ni kwamba rushwa imekuwa kubwa sana Mahakama ya Mwanzo Nunge na haki za wananchi wasio kuwa na pesa kuporwa na kinachofanywa ni kupindisha uamuzi wa kesi mbalimbali.

Sisi, kama whistleblowers tunaomba Msajiri wa Mahakama kuu Morogoro tupia jicho kesi zote kutoka mahakama hiyo, inaharibu image ya Mahakama.

Ili kujihakikishia mahakama fanyeni uchunguzi kwa kushirikiana na TAKUKURU, mtagundua mengi na mtakuwa mmesaidia kuokoa haki za watu zinazoporwa kwa rushwa mahakamani hapo.
Msajili wa Mahakama Kuu yeye mwenyewe ndio mla rushwa Namba Moja katika Mahakama ya Tanzania.
Hao Wasajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro ni tatizo kubwa sana, rushwa hapo inatembezwa nje nje, Wala hakuna kificho. Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro inanuka rushwa, imeoza kabisa, kama hauna rushwa jiandae kudhulumiwa haki yako.
 
Mahakama zote ni rushwa tupu hakuna haki
Hata kwenye Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya nako hali ni mbaya zaidi. Hapo Baraza la Ardhi la Wilaya ya Morogoro kuna huyo Hakimu wa kiume ndiyo janga kubwa zaidi, amekuwa akipokea rushwa wazi wazi, Mawakili ndio watu wake ambao wamekuwa wakimpelekea rushwa.
 
Wanapata ajira kwa rushwa hivyo lazima wapokee rushwa wazi wazi
 
Back
Top Bottom