Morogoro: TANROADS yasema ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami Rudewa-Kilosa (Kilometa 24) umefikia 90%

Morogoro: TANROADS yasema ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami Rudewa-Kilosa (Kilometa 24) umefikia 90%

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami Dumila-Kilosa-Mikumi sehemu ya Ludewa-Kilosa yenye urefu wa kilometa 24 umefikia asilimia 90 ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika Julai, 2023.

Kazi iliyobakia ni ujenzi wa madaraja matatu huku ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ikiwa imekamilika na kuendelea kutumika.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Mussa Kaswahili amesema hayo akitembelea miradi ya Ludewa-Kilosa na daraja la Kiyegeya lililopo Wilayani Gairo ambapo amesema barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya mkoa huo ambayo inaanzia Dumila hadi Mikumi.
Mhandisi Mussa Kaswahili.jpg

Mhandisi Mussa Kaswahili​

Mhandisi Kaswahili ameongeza kuwa, hapo awali watumiaji wa barabara hiyo walikuwa wanatumia muda mrefu barabarani hadi kufika wakitokea Dumila kwenda Rudewa au Kilosa kutokana na ubovu wa barabara iliyokuwepo.

"Hapo awali kabla ya ujenzi wa barabara ya Dumila hadi Kilosa, ilikuwa kutoka Dumila hadi Ludewa ilikuwa ni saa tatu lakini kwa sasa ni takribani dakika 40 tu unakuwa umefika," alisema Mhandisi Kaswahili.

Ameendelea kwa kusema kuwa, mradi wa Ludewa-Kilosa ulibuniwa ili kuwajengea uwezo wakandarasi wazawa katika kuongeza ushiriki wako kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu.

Wakiongea kwa nyakati tofauti, Meneja wa mradi kutoka Kampuni ya ushauri ya Pidael JV Consulting Engineers Mhandisi Protas Mwasyoke na msimamizi wa mradi upande mkandarasi, Mhandisi Leons Msoka wamesema kwa mwenendo wa kazi za ujenzi zinavyoendelea na kwa kazi ikiyobakia ya ujenzi wa madaraja matatu, kazi hiyo itakamilika kwa wakati mwezi Julai, mwaka huu.
 
Mradi huo umechelewa sana,kilosa ilitakiwa miaka mingi lami ishaingia

Ova
 
Back
Top Bottom