Morogoro town centre yakumbwa na mafuriko ya tope

Morogoro town centre yakumbwa na mafuriko ya tope

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
March 7, 2020
Morogoro, Tanzania

Mvua kubwa iliyonyesha milima ya Uluguru inayoizunguka mji kasoro bahari wa Morogoro umejikuta wakazi na wafanyabishara wa mjini kati yaani down town city centre ukiwa na mafuriko ya tope jingi na maji. Wakazi waomba miundo mbinu ya mifereji na mto unaokatiza katikati ya mji ifanyiwe marekebisho

Source: Mcl digital
 
Sasa naelewa kwanini mkoloni aliamua ofisi za Boma, Morogoro Hotel n.k kuwa maeneo yaliyoinuka ya mjini Morogoro. Mkoloni aliisoma jiografia ya eneo husika kabla ya kuamua wapi majengo muhimu ya kiutawala na makazi yawepo.

Tatizo halmashauri nyingi zinafanya mipango miji yao kwa kutumia macho na maelekezo ya wanasiasa wasioelewa mipango miji, badala ya kufanya utafiti kwa kutumia wataalamu kama wa Chuo Kikuu cha Ardhi au kusoma makabrasha ya mkoloni ili kubaini siri ya maeneo ya 'uzunguni' kutopatwa na madhara ya mafuriko n.k

19 February 2020

MIKAKATI YA MRADI ULGSP KUBORESHA MJI WA MOROGORO

Source : OR TAMISEMI
 
Poleni sana Moro. Video inasikitisha sana wananchi wanavyolalamika.

Wengine wanasema mto ufanyiwe diversion, wengine wanalalamika crisis kwenye confidence ya kununua vitu, simu hazitanunulika ikiwa watu watafikiri zimeingiliwa na tope, wengine wanalalamika wamekopa hela za biashara na hali hii itawaletea ugumu kulipa.

Meneja anajitetea tatizo si miundombinu, ni mvua kubwa. Kwani miundombinu kama imepangwa kuhimili mvua kubwa ingeshindwa?
 
Limebusurika?Kiluguru au?

Njoo Matombo njiapanda Mission na Mtamba.

Baadae twende zetu Mtombozi mbele ya Mtamba na Kangazi.

Mweeee!!Ulonga choni??

Kuna mwali ananemwa huku karibu na kwa Mzee(Rip) Zegele!!

Hehehehehe!!!
Dah poleni sana hometown vp lile soko letu jipya la mwaka 1953 limebusurika?! maana lipo karibu na mto ule!
 
Limebusurika?Kiluguru au?

Njoo Matombo njiapanda Mission na Mtamba.

Baadae twende zetu Mtombozi mbele ya Mtamba na Kangazi.

Mweeee!!Ulonga choni??

Kuna mwali ananemwa huku karibu na kwa Mzee(Rip) Zegele!!

Hehehehehe!!!

hahahaha kunusurika... shekhee moro ndio home mie
 
Miradi mingi ya serikali kama wananchi wangeshirikishwa, wangetoa vipaumbele vyao.

Mfano mji wa Morogoro au Dar es Salaam miradi ya vituo vipya vya mabasi yaendayo mikoa mingine wangeikataa. Badala yake wangependa pesa hizo zielekezwe kujenga na kuboresha mifumo ya mifereji ya maji machafu na barabara za mitaani mwao.

Lakini kwa kutaka sifa za Maendeleo ya Vitu badala ya Maendeleo ya Watu kupitia huduma za jamii zinazogusa wengi kama mifumo ya maji safi, taka, wataalamu wa afya, zahanati, shule, waalimu na mitaa ya barabara bora xilizojengwa kwa mawe au lami serikali kuu inakazania Miradi ya Vitu vikubwa kuonesha inafanya makubwa lakini ukweli miradi hiyo ya Vitu Vitu vikubwa hawagusi maisha ya kila siku ya mwananchi mitaani au vijijini.
 
March 7, 2020
Morogoro, Tanzania

MAFURIKO MOROGORO: Wodi za Wagonjwa Zajaa Maji, MIGAHAWA MADUKA YAFUNGWA

Kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro, wananchi wa Morogoro wamejikuta katika wakati mgumu baada ya nyumba zao na maaneo ya kazi kujaa maji na kusimamisha huduma kusimama.

Source: Global TV online
 
Somo lako linaendelea au limeishia hapa tupe na ya idodomia
Sasa naelewa kwanini mkoloni aliamua ofisi za Boma, Morogoro Hotel n.k kuwa maeneo yaliyoinuka ya mjini Morogoro. Mkoloni aliisoma jiografia ya eneo husika kabla ya kuamua wapi majengo muhimu ya kiutawala na makazi yawepo.

Tatizo halmashauri nyingi zinafanya mipango miji yao kwa kutumia macho na maelekezo ya wanasiasa wasioelewa mipango miji, badala ya kufanya utafiti kwa kutumia wataalamu kama wa Chuo Kikuu cha Ardhi au kusoma makabrasha ya mkoloni ili kubaini siri ya maeneo ya 'uzunguni' kutopatwa na madhara ya mafuriko n.k

19 February 2020

MIKAKATI YA MRADI ULGSP KUBORESHA MJI WA MOROGORO

Source : OR TAMISEMI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni sana Moro. Video inasikitisha sana wananchi wanavyolalamika.

Wengine wanasema mto ufanyiwe diversion, wengine wanalalamika crisis kwenye confidence ya kununua vitu, simu hazitanunulika ikiwa watu watafikiri zimeingiliwa na tope, wengine wanalalamika wamekopa hela za biashara na hali hii itawaletea ugumu kulipa.

Meneja anajitetea tatizo si miundombinu, ni mvua kubwa. Kwani miundombinu kama imepangwa kuhimili mvua kubwa ingeshindwa?

Maelezo ya wananci yana make sense kuliko maelezo ya meneja.
 
Maelezo ya wananci yana make sense kuliko maelezo ya meneja.
Unaona sasa?

Asante sana mwana.

Hata mimi niliona hivyo, ila nikawa najipa nafasi ya kuwa labda kuna kipande nimekosea.

Meneja kajibu maswali magumu kwa hoja nyepesi sana.

Labda alihojiwa bila kuona maelezo ya wananchi, inabidi ajipange upya na wakubwa zake kuweka mkakati na kujibu hoja za wananchi.
 
Angehojiwa baada ya kusikiliza mapni ya wananci akili ingemshutka.

Nakubaliana nawe jamaa kahojiwa pasipo kujua wananchi wanafikiria nini.
Kaonyesha upeo wake wa kufikiri ulipoishi, kulaumu mvua badala ya kuongelea kiini cha tatizo na mipango ya endelevu ya kukabiliana na tatizo.

Nikuambie kitu, tatizo ni elimu inayotolewa mashuleni kwetu, haichochei ubunifu na utatuzi wa matatizo ya kijamii.

Sishangai mkuu ana order ndege badala ya kujenga maabara na kuziwekea vifaa vya kisasa, kufadhili tafiti na kuchochea machapisho na uandishi wa vitabu.

Mkuu na timu yake wamekosa kujua vichochezi vya maendeleo na vinavyohitaji kupewa kipaumbele.

Kwa hali hii tutaendelea kupiga mark time kwenye maendeleo endelevu na tutaendelea kuyasikia nchi jirani na ng'ambo.
 
Back
Top Bottom