Poleni, lakini picha wapi?
Dah poleni sana hometown vp lile soko letu jipya la mwaka 1953 limebusurika?! maana lipo karibu na mto ule!
Limebusurika?Kiluguru au?
Njoo Matombo njiapanda Mission na Mtamba.
Baadae twende zetu Mtombozi mbele ya Mtamba na Kangazi.
Mweeee!!Ulonga choni??
Kuna mwali ananemwa huku karibu na kwa Mzee(Rip) Zegele!!
Hehehehehe!!!
Sasa naelewa kwanini mkoloni aliamua ofisi za Boma, Morogoro Hotel n.k kuwa maeneo yaliyoinuka ya mjini Morogoro. Mkoloni aliisoma jiografia ya eneo husika kabla ya kuamua wapi majengo muhimu ya kiutawala na makazi yawepo.
Tatizo halmashauri nyingi zinafanya mipango miji yao kwa kutumia macho na maelekezo ya wanasiasa wasioelewa mipango miji, badala ya kufanya utafiti kwa kutumia wataalamu kama wa Chuo Kikuu cha Ardhi au kusoma makabrasha ya mkoloni ili kubaini siri ya maeneo ya 'uzunguni' kutopatwa na madhara ya mafuriko n.k
19 February 2020
MIKAKATI YA MRADI ULGSP KUBORESHA MJI WA MOROGORO
Source : OR TAMISEMI
hahahaha kunusurika... shekhee moro ndio home mie
Nimepita sana huko.Dada zako wana sura ngumu kweli na sio wachoyo hata kidogo na miguu yao yenye vigimbi,mfano wa kule Tawa.
Poleni sana Moro. Video inasikitisha sana wananchi wanavyolalamika.
Wengine wanasema mto ufanyiwe diversion, wengine wanalalamika crisis kwenye confidence ya kununua vitu, simu hazitanunulika ikiwa watu watafikiri zimeingiliwa na tope, wengine wanalalamika wamekopa hela za biashara na hali hii itawaletea ugumu kulipa.
Meneja anajitetea tatizo si miundombinu, ni mvua kubwa. Kwani miundombinu kama imepangwa kuhimili mvua kubwa ingeshindwa?
Unaona sasa?Maelezo ya wananci yana make sense kuliko maelezo ya meneja.
Unaona sasa?
Asante sana mwana.
Hata mimi niliona hivyo, ila nikawa najipa nafasi ya kuwa labda kuna kipande nimekosea.
Meneja kajibu maswali magumu kwa hoja nyepesi sana.
Labda alihojiwa bila kuona maelezo ya wananchi, inabidi ajipange upya na wakubwa zake kuweka mkakati na kujibu hoja za wananchi.