Morogoro: Watoto zaidi ya 1200 wapatiwa ujauzito ndani ya mwaka mmoja

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Afisa Ustawi wa Jamii mkoani Morogoro, Jesca Kamugela amesema Matukio ya mimba na ndoa za utotoni yamezidi kuongezeka katika mkoa huo ambapo katika kipindi cha mwaka mmoja 2020/21 ya watoto 1,277 wamepata ujauzito kulingana na matukio yaliyoripotiwa.

Halmashauri zote za Morogoro zimekuwa zikiripoti matukio hayo na hali imeendelea kutokuwa nzuri. Jesca amesema chanzo kikubwa wanachokiona ni mmomonyoko wa maadili hasa kwa upande wa wazazi na hata watoto.

Najiuliza pamoja na sheria kali ya kumpa ujauzito mwanafunzi lakini wapi, tufanyaje kama jamii?
 
Hatari Halafu Hao Watoto Wanarudi Kuwa Tegemezi Kwa Wazazi
 
Hao watoto ni wapo wenye Miaka 17? Maana mpaka sasa Sheria bado haijabadili mtoto wa Miaka 17 kuolewa. Isijekuwa wa umri huo kaipatia mimba ndoani halafu ahesabikie mtoto kapata mimba.
 
Duh hii ni hatari, ingefaa kwa wazazi waanze kutoa funzo la maadili kwa watoto maana huo mmomonyoko unaonekana ni mkubwa sana.
 
Kukosa hofu ya Mungu
Singeli zimezidi
Bange
Boda boda
Njaa
Elimu ndogo kutoka kwa wazazi
Ongezeko la vijana wa magetoni
Tamaa
Fashion (kubebesha mimba)
Na nyingine kama hizo yani ni tafran
Hahaha [emoji23], ila Morogoro ndani ndani kule watu wanapenda sana vigodoro aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…