Morogoro: Watu 3 wakamatwa kwa tuhuma za kufukua maiti na kunyofoa viungo

Morogoro: Watu 3 wakamatwa kwa tuhuma za kufukua maiti na kunyofoa viungo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Watu watatu wanashikiliwa na Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kufukua mwili wa Rehema Michel, aliyezikwa Jumapili na kutoa viungo mbalimbali ikiwamo kichwa, figo na sehemu za siri.

Mwili wa marehemu Rehema ulizikwa kwenye makaburi ya familia katika Kijiji cha Nguyami, Kata ya Idibo wilayani Gairo mkoani Morogoro.

Akizungumza na Mwananchi juzi, Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Fotunatus Musilimu alisema tukio hilo lilitokea jana alfajiri katika eneo ambalo ni umbali wa mita 50 kutoka kwenye makazi ya watu kijijini hapo.

Musilimu alisema taarifa za awali zilieleza kwamba mwanamke huyo (35) alipata ajali mjini Morogoro na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro na siku chake baadaye alifariki dunia.

Alisema mwili wa mwanamke huyo ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti hospitalini hapo na Mei 23, 2021 (Jumapili) ulisafirishwa na kuzikwa siku hiyo. “Baada ya kumaliza mazishi, leo alfajiri (juzi) kulipokucha wakakuta kaburi limefukuliwa na mwili umetolewa kwenye sanduku.

Mwili ulikutwa umekatwa badhi ya viungo ambavyo ni kichwa, sehemu za siri, shingo, mkono na mguu wa kushoto na kuupasua mwili na kuchukua pafu la kushoto na moyo,” alisema.

Mwananchi
 
Imani za kishirikina ni tatizo kubwa sana katika jamii zetu za kia Afrika.

Ugumu wa kunyofoa maiti viungo unazidi ugumu wa kuua. Hao jamaa ni makatili sana.
 
Yaani wanakata kama nyama ya ngo'mbe dah!
 
Ni sababu Afrika maendeleo ni duni kisa imani za kishirika kutawala kila sekta.
 
Ushirikina ni dhuluma kubwa sana,
Jitihada ya ziada inahitajika ili kuokoa viumbe na ushirikina
 
Maisha yamekuwa magum mpk watu tumegeuka wanyama hatuna utu teena.
 
"na kuupasua mwili kuchukua pafu la kushoto na moyo" kuna watu wana roho ngumu sana..
 
Gairo huko wakaguru ni haataarrriii!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mmh jamani mbona ni ukatili sana huu, ushirikina unapelekea watu wafanye vitu vya kushangaza na kuhuzunisha.sad!
 
Hivi ni kweli kwamba waafrica walikuwa wanyama ?
kitabu cha tiptip kama unakifahamu (alikuwa mwenye asili pwani na bara) jina halisi limenitoka kidogo

Anaelezea safari zake za kibiashara na matukio ya hatari na kustaajabisha aliyopitia mnamo karne ya 19 afrika mashariki na kati

Moja ya tukio la kusisimua alilosimulia ni baada ya yeye kufanikiwa kukutana na kaka wa bibi yake ambaye alikuwa ni chifu mkubwa sana(huku bara)

Kisha akamuomba kwa hila ashirikiane nae katika uvamizi wa kaya nyengine ili yeye(tiptip) aweze kunafaika kibiashara kwa ukusanyaji wa pembe za ndovu_akakubali

Anesema mwenyewe kwa maneno yake ilikuwa ni kwa kiasi gani aliumizwa kuona aliotoka kuwatambua kama ni ndugu zake kumbe nao ni wala watu.!

Ilikuwa ni kila mji wanaoupiga na maiti kutapakaa, kwenye moto wa jioni wale washenzi (jina la watu wasiostaarabika wa bara) ambao pia ni ndugu zake walikuwa wanabanika wale maadui zao wa kivita na kisha wanawala.!

Hilo likawa linamuumiza akawa anajaribu kuwasihi wasifanye hivyo nao wakamjibu ''akitaka wasifanye hayo kwenye raha ya mlo wao, naye awache kula mbuzi na vitoweo vyote anavyovifurahia kuvila ili iwe 50/50'' na anasema kwa msisitizo washenzi wawili wanauwezo wa kumla mtu mmoja peke yao.!

Si miaka mingi sana takriban 200 na ushee hayo yalikuwa ni kawaida sana huku kwetu afrika na kwakuwa vitabu kama hivi vilizuiwa kufundishia historia ya kweli basi watoto wa siku zetu wanadhani africa ilitawaliwa kwa bahati mbaya
 
Back
Top Bottom