Morrison kupewa ushindi,wachambuzi maandazi leo limewashuka

Morrison kupewa ushindi,wachambuzi maandazi leo limewashuka

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Hutasikia mtu anaongelea majibu ya uchunguzi wa polisi.

Ukweli ni kwamba Yanga ilighushi saini ya Morrison. Hili ni kosa kubwa sana na wanastahili kushushwa daraja.

Bado inaonesha mchezo mchafu huo ulifanywa kwa ushirikiano na baadhi ya watendaji wa TFF.Kuna umuhimu wa kufanya uchunguzi huru kujua nini kilitokea hapo TFF kuwezesha ujinga waliofanya Yanga hadi wakaamini wako sahihi.

Wachambuzi wataishia kulaumu vilabu vya Simba na Yanga huku ushahidi unaonesha kuwa Yanga ndiyo inaendeshwa kihuni sana.

Jiulize kauli yao kuhusu Shishimbi kusaini mkataba wa mwaka miwili.

Jiulize kuhusu barua yao waliyojiita sure boy na mchezaji akawakana.

Wachambuzi maandazi yote hayo huwezi kuwasikia wakiyasema.
 
Kitenge Leo anaweweseka tu, ningekua na namba ya Ambangile ningemshauri aendelee na weledi huo huo, maana alikua anakataa kulisemea suala hilo kwa sababu hakuna mwenye makosa.

Lakini akina kitenge na uyanga wao walikua wanamuona Morison muongo, sasa wameumbuka
 
Hata washabiki wa yanga hawawezi kuwasema chochote GSM waliowaingiza chaka. hata ishu za Laliga kuna chenga nyingi sana.
 
Yaani kuna mwanamichezo halisi anashabikia upuuzi uliojitokeza katika suala hili? Uwe unamuunga mkono Morison au unaunga mkono Yanga basi hujitambui.
 
Yaani kuna mwanamichezo halisi anashabikia upuuzi uliojitokeza katika suala hili? Uwe unamuunga mkono Morison au unaunga mkono Yanga basi hujitambui.
Sehemu yoyote ambapo binadamu wanaishi lazima conflict zitokee, hata wewe inawezekana na mke au Mme wako, ndugu zako mnaingia kwenye conflict, lakini mnatafuta suluhisho.

Hakuna anayeshabikia mgogoro ila tulikua tunataka haki itendeke, sio kumhukumu mtu bila kumsikiliza.
@ Usinifokee
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Back
Top Bottom