MORUWASA: Tuna upungufu wa uzalishaji maji kwa 49% ndio maana Morogoro kuna mgao

MORUWASA: Tuna upungufu wa uzalishaji maji kwa 49% ndio maana Morogoro kuna mgao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira wa MORUWASA, Mhandisi Thomas Ngulika akielezea hali ya upatikanaji wa maji katika Manispaa ya Morogoro amesema changamoto kubwa inayosababisha upungufu wa maji Mkoani hapo ni uzalishaji mdogo mbao hauendani na mahitaji husika

Amesema “Mahitaji ya maji kwa Morogoro ni Lita Milioni 81 kwa siku lakini uzalishaji ni Lita Milioni 41 kwa siku, tunazalisha Asilimia 51 kwa siku, hivyo kuna upungufu wa Asilimia 49, hali hiyo inasababisha tutoe huduma yetu kwa mgao.”

Amesema hayo baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kuhoji juu ya uhaba wa maji huku kukiwa na ukimya wa MORUWASA.

Kusoma hoja ya Mdau bofya hapa ~ Waziri Aweso unasema DAWASA kuna hujuma? Njoo Morogoro, huduma ya Maji ni kero kubwa
 
Na mito yote iliyoko Morogoro, pia mvua yote iliyonyesha wanashindwa kuhifadhi maji?
 
Back
Top Bottom