chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Ile ajenda ya Kodi za zamani aliyoisema Mh. Rais na Mbunge wa Bukoba Mjini ni taa ya kukaa sawa dhidi ya Moses Machali, mkuu wa wilaya ya Bukoba, kwamba "walangila wameshamkalia vikao, na hawamtaki".
Bukoba ni wilaya ambayo Siasa imetamalaki, na Kuna wafanyabiashara wameshamuunguzia Uzi, na wanasiasa wanamuona anaharibu upepo wa kisiasa.
Kwa kifupi, anaweza kuhamishwa au kutupiwa virago.
Zile Kodi za leseni za biashara ulizoanza kuwapigia, kodi za miaka kadhaa nyuma, ukamdaka Afisa Biashara .....na mengineyo, na "kuwanyanganya" maduka wale wazee pale soko kuu, na kuwapangisha wapangaji, ni jambo jema, lakini hao jamaa " wanachoma utambi" balaa kwa kukunanga na "kukusimanga" kisiasa, na ushindi wao ni wewe kuondolewa Kagera.
Hiyo ndio Kagera, wenyewe Wana msemo wao " ukija Kagera ukaondoka hujaharibikiwa, mshukuru Mungu".
Kwa hisani ya wanywa kahawa soko kuu Bukoba