Moses Phiri asingemuweka Fiston Mayele Kichwani mwake haya Majeraha asingeyapata

Moses Phiri asingemuweka Fiston Mayele Kichwani mwake haya Majeraha asingeyapata

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kinachomgharimu Moses Phiri ni kutokubali kwanba Mshindani wake Fiston Mayele yuko kwenye Njia ( Relini ) Kiufungaji kutokana na Kuizoea Ligi Kuu ya Tanzania kulko Yeye Mgeni.

Matokeo yake sasa Moses Phiri analazimika kutumia Nguvu Kubwa Kushindwana Kiufungaji n Fiston Mayele matokeo yake maeneo mengine anashindwa kuchukua na kujikuta ama anaumia au anaumizwa.

Kitu pekee ninachokiona kwa Fiston Mayele na ambacho namshauri Moses Phiri akiige ni kwamba pamoja na kwamba Mayele anakitaka Kiatu cha Dhahabu ila Yeye anacheza zaidi kwa kuipambania Yanga SC yake ipate Matokeo halafu Kufunga Kwake Magoli ni baadae.

Kwa Moses Phiri yeye hata ukimtizama tu akicheza na hasa akisikia labfa Jana Mayele amefunga basi atahangaika kutaka nae afunge Goli Kilazima hata kama Nafasi ni Nadra badala ya Kucheza kwa ajili ya Simba SC ( nikimaamisha hata asipofunga Yeye ) bado cha muhimu ni Simba SC ipate Alama / Ushindi.

Nina uhakika Benchi la Ufundi la Simba SC lingemwambia Moses Phiri kuwa asiwe anapenda sana Kukaa na Mpira, kufanya Dribling mno na Kulazimisha kupita kwa Mabeki Makatili na Wengine wenye DNA zote za Yanga SC ( Kuishabikia ) Yanga SC wala asingeumizwa hivi alivyoumiza na huu ni Uzembe mkubwa katika Technical Bench la Simba SC likiongozwa na Kocha Mkuu Juma Mgunda.

Pole yake ila akipona tu awe Makini.
 
hii mbona kama promo kwa Mayele na dongo kwa Phiri na mbumbumbu fc wote , dizaini kama vile Genta kavaa uzi wa wananchi!! Au kahamia jangwani coz msimbazi pameoza hapasomeki na Barabara katimka?
 
Back
Top Bottom