Moshi: Kijana akutwa amefariki dunia shambani huku mwili wake ukiwa hauna nguo

Moshi: Kijana akutwa amefariki dunia shambani huku mwili wake ukiwa hauna nguo

Kijana mmoja ajulikanae kwa jina la Emmanuel Alex, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28, amekutwa amefariki dunia shambani huku mwili wake ukiwa hauna nguo yoyote.

Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Orori kata ya Machame Mashariki, limezua taharuki miongoni mwa watu katika eneo hilo huku chanzo cha kifo kikiwa bado hakijajulikana.

Polisi walifika eneo la tukio na kuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya Uchunguzi zaidi.
Huyo atakuwa kapiga cha Arusha chaliiii waaangu iseeeee!
 
Moshi ndo mji pekee wenye majambazi sugu mahuligani na walevi wakutosha

Sitasahau siku majambazi yalinivaa mitaa ya PASUA yalikuwa manene marefu afu panga ndefu kama ulimi wa twiga.. Nilibak na nguo tu nilizovaa [emoji1374]
Nimecheka mpaka basi, sasa wangezitaka hadi nguo sijui ungefikaje Dodoma Mpwayungu.
 
Moshi ndo mji pekee wenye majambazi sugu mahuligani na walevi wakutosha

Sitasahau siku majambazi yalinivaa mitaa ya PASUA yalikuwa manene marefu afu panga ndefu kama ulimi wa twiga.. Nilibak na nguo tu nilizovaa [emoji1374]
Mkuu aukuleta ule ubaunsa kama ulivyo wafanyia wale mabaunsa wa wauza uchi?
 
Kijana mmoja ajulikanae kwa jina la Emmanuel Alex, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28, amekutwa amefariki dunia shambani huku mwili wake ukiwa hauna nguo yoyote.

Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Orori kata ya Machame Mashariki, limezua taharuki miongoni mwa watu katika eneo hilo huku chanzo cha kifo kikiwa bado hakijajulikana.

Polisi walifika eneo la tukio na kuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya Uchunguzi zaidi.
Kwamba tukio hili ni la Ajabu?
Katika vitabu vikuu kumeandikwa kuwa(imetolewa ahadi) tutazaliwa na tutakufa na hakuna sehemu inayosema utazaliwa na nguo au lah, na katika maisha yangu sijawahi kusikia mtu au mtoto kazaliwa na nguo! Nini cha ajabu kukutwa mtu amekufa akiwa hana nguo?
(its a rhetoric question)

Ninachotaka kusema ni kwamba tunapopeana taarifa hatuna ulazima wa kuyakuza maneno, hasa linapokuja suala la kupeana taarifa ya msiba.

Poleni wafiwa wote.
R.I.P Emmanuel Alex, ulikuja kwa Udongo umekwenda kwa Udongo.
 
Kwamba tukio hili ni la Ajabu?
Katika vitabu vikuu kumeandikwa kuwa(imetolewa ahadi) tutazaliwa na tutakufa na katika maisha yangu sijawahi kusikia mtu au mtoto kazaliwa na nguo! Nini cha ajabu kukutwa mtu amekufa akiwa hana nguo?
(its a rhetoric question)

Ninachotaka kusema ni kwamba tunapopeana taarifa hatuna ulazima wa kuyakuza maneno, hasa linapokuja suala la kupeana taarifa ya msiba.

Poleni wafiwa wote.
R.I.P Emmanuel Alex, ulikuja kwa Udongo umekwenda kwa Udongo.
Je, una uelewa wowote ule (basic knowledge) kuhuau masuala ya CRIMINOLOGY au Criminal Intelligence??
 
Teacher mpyayungu unavyowasagia walimu wenzako kama vile we ni waziri au mkurugenzi flan hivi.Kwahiyo kifo Kwa walimu wenzako kwako kicheko.
Jamaa anafake life hadi anaboa,kwanini kila uchao anawasagia kunguni walimu?
Sio fear hata kidogo mana sote hapa tumepita mikononi mwao.
Inasikitisha kiukweli ona sasa anacheka eti alidhani mwalimu amedanja sio poa man mimi nina ndugu walimu so hata kama kipato kidogo lakin sio kuwapopoa kila Mara unajishushia heshima.
 
Je, una uelewa wowote ule (basic knowledge) kuhuau masuala ya CRIMINOLOGY au Criminal Intelligence??
Hapana, ila nitashukuru ukinielewesha. Inasemaje, kwamba ukikutwa umekufa bila nguo ina maana gani?

Naelewa unakuja kwa udongo na unaondoka kwa udongo, hakuna anaezaliwa akiwa amevaa nguo na hakuna ajabu yeyote ile mtu akifa akiwa uchi!

Poleni wafiwa.

R.I.P Emmanuel Alex

.
 
Back
Top Bottom