Moshi, Kilimanjaro: Mwanamke auawa kwa kuchinjwa, Polisi yasema kuna viashiria vya visasi

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Moshi. Elice Matafu, Mkazi wa Kijiji cha Mrimbo Uuwo, Kata ya Mwika Kaskazini, Wilaya ya Moshi ameuawa kwa kukatwa shingo na watu wasiojulikana nyumbani kwake.

Mwanamke huyo ameuawa usiku wa saa 2 akiwa nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kuuawa kwa mwanamke huyo na amesema mauaji hayo yanaviashiria vya visasi ambapo tayari anashikiliwa kijana mmoja kwa mahojiano zaidi.

"Ni kweli huyu mwanamke ameuliwa nyumbani kwake usiku kwa kukatwa shingo na inaonekana kuna viashiria vya visasi, tayari tunamshikilia kijana mmoja kwa mahojiano zaidi,"amesema Kamanda Maigwa.

Kamanda Maigwa amesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini hasa chanzo cha mauaji hayo.
 
Hao watu wa Kas. kwa pesa, wako tayari kufanya lolote.

R.I.P. Elice

Kamanda, pole kwa majukumu.
 
Si mbaya wakajua tukio la Hamza hawaaminiki kwani wao pia ni sehemu ya watuhumiwa
Tukio la Hamza limewakalia vibaya Sana, we subir report itoke, utasikia alikua kwenye kikosi Cha aliqaida!

Sasa, Gaidi gani anayewaacha raia salama kabisaaah bila kuwafanya chochote, huku akionesha Nia yake Ni police TU! Pale Kuna inshu ya visasi Kama hii ilivyorepotiwa, tofauti Ni kwamba ile polisi ndye chanzo Cha uhasama!
 
Hamza anasemekana alikuwa na kikaratasi chenye maelezo yote.

Watakikana, kitabadilishwa to justify the end.

Hiyo ndiyo polisi ya Sirro.
 
Kwahiyo tumekubaliana kwamba Hamza mtandao wake uko nchi nzima si ndio? sasa mmekosea alitakiwa hilo tukio lihamishiwe kule Hai ili kuunganisha Dot za UGAIDI wa MBOWE
 
Moshi. Elice Matafu, Mkazi wa Kijiji cha Mrimbo Uuwo, Kata ya Mwika Kaskazini, Wilaya ya Moshi ameuawa kwa kukatwa shingo na watu wasiojulikana nyumbani kwake.

Mwanamke huyo ameuawa usiku wa saa 2 akiwa nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kuuawa kwa mwanamke huyo na amesema mauaji hayo yanaviashiria vya visasi ambapo tayari anashikiliwa kijana mmoja kwa mahojiano zaidi.

"Ni kweli huyu mwanamke ameuliwa nyumbani kwake usiku kwa kukatwa shingo na inaonekana kuna viashiria vya visasi, tayari tunamshikilia kijana mmoja kwa mahojiano zaidi,"amesema Kamanda Maigwa.

Kamanda Maigwa amesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini hasa chanzo cha mauaji hayo.
Ila ya Hamza haikuwahi kuwaziwa kwamba ni visasi?
 
Back
Top Bottom