Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi imeahirisha usikilizwaji wa mashahidi wa upande wa mashtaka katika kesi ya makosa ya mtandao inayomkabili Mchungaji Godfrey Malisa, baada ya mshtakiwa kuomba kuahirishwa kwa shauri hilo akisubiri msaada wa kisheria kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
Jumatano, Februari 11, 2026, mahakama ilikuwa imepanga kusikiliza mashahidi wawili wa upande wa mashtaka, lakini Malisa aliomba kuahirishwa kwa kesi hiyo akieleza kuwa wakili wake hayupo kwa kuwa anasubiri idhini kutoka makao makuu ya TLS ili aweze kumwakilisha mahakamani.
Hakimu Mkazi Ally Mkama, anayesimamia kesi hiyo, alimweleza Malisa kuwa hili ndiyo ahirisho la mwisho na kwamba usikilizwaji wa kesi lazima uanze leo Alhamisi, Februari 12, 2026.
Hakimu alifafanua kuwa kesi tano nyingine za madai ziliahirishwa Jumatano ili mahakama iweze kuipa kipaumbele kesi hii ya jinai, akibainisha kuwa kesi kama hii zinaendelea katika mahakama nyingine.
“Pindi kesi zinapofikishwa mahakamani, ni lazima zisikilizwe ikiwa mahakama ina mamlaka. Hii ndiyo kesi pekee ambayo bado haijaanza kusikilizwa. Ninatoa ahirisho la mwisho. Kesho (Alhamisi, Februari 12, 2026) saa 3 asubuhi, lazima ufike. Kesi lazima iendelee,” alisisitiza.
Mahakamani ilibainika kuwa ombi la Malisa la kupata msaada wa kisheria liliwasilishwa, Jumanne, Februari 12, 2026, kwa chama cha mawakili Moshi, ambao wamewasiliana na makao makuu kuidhinisha wakili, kwa kuwa pia anakabiliwa na kesi ya uhaini.
UPDATES
Baada ya ahirisho la Februari 11, kesi hiyo ilianza kusikilizwa Feruari 12, ambapo shahidi wa kwanza alianza kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi, Ally Mkama, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.
Akizungumza Februari 13, 2026, Rais wa TLS, Wakili Boniface Mwabukusi, alisema tayari wameshaingia kwenye kesi hiyo kwa kuteua mawakili kutoka Chapter ya Kilimanjaro ni Leonard Mashabara, Deogratias Matata, Elisante Kimaro, Moonlight Tupa na Fredy Kimaro.
Alisema baada ya shajidi wa kwanza kusikilizwa iliahirishwa hadi Februari 20, 2026 kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji.
Zaidi soma

- Dkt. Malisa: Rais Samia ajiuzulu kabla ya Disemba 9 au Akabili Maandamano makubwa ambayo hayajawahitokea Barani Afrika
- Aliyekosoa mchakato wa uteuzi wa Samia ndani ya CCM, Mzee Godfrey Malisa ashtakiwa kwa UHAINI
- Mbali na kesi ya Uhaini, Dkt. Malisa afunguliwa pia kesi ya Jinai ya Makosa ya Kimtandao
- Inadaiwa Dkt. Godfrey Malisa ametekwa jana usiku akiwa nyumbani kwake