Moshi: Mwalimu wa hisabati jela maisha kwa kulawiti mwanafunzi

Uzi huu utakuwa na kurasa chache sana! Mleta mada kuna sehemu umefeli.....
 
Mahakama ya Rufani imebariki kifungo cha maisha alichohukumiwa mwalimu wa Shule ya Msingi Chomvu iliyopo Wilaya ya Mwanga, Elibariki Mchomvu kwa kulawiti mwanafunzi wake wa kiume mwenye umri wa miaka tisa.

Mchomvu, aliyekuwa akifundisha hisabati, alipatikana na hatia kwa mara ya kwanza mwaka 2019 ya kumlawiti mwanafunzi huyo chooni na kuhukumiwa na hakimu mkazi Mwanga, Mariam Lusewa kifungo cha miaka 30 jela.

Hata hivyo, mwaka huohuo akakata rufaa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi kupinga adhabu hiyo, lakini Jaji Susan Mkapa si tu kwamba alitupilia mbali sababu zake za rufaa, lakini aliongeza adhabu na kuwa kifungo cha maisha.

Hakuridhika na kukata tena rufaa Mahakama ya Rufani Tanzania, jopo la majaji watatu walitoa hukumu na kubariki kifungo hicho cha maisha jela.

Mfungwa huyo aliwasilisha hoja 10 kupinga kutiwa hatiani na adhabu ambazo hata hivyo zilipanguliwa na upande wa jamhuri ukiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Verdiana Mlenza aliyesaidiana na wakili Sabitina Mcharo.

Katika hukumu yao iliyotolewa wiki iliyopita na nakala ya hukumu kupatikana jana,majaji hao, Dk Gerald Ndika, Ignas Kitusi na Omar Makungu walisema sababu za rufaa hazikuwa na mashiko na kubariki adhabu hiyo.

“Kwa kuzingatia kuwa mlalamikaji alikuwa na umri wa miaka tisa wakati wa tukio, Mahakama Kuu Moshi ilikuwa sawa kuingilia kati na kutoa kifungo sahihi cha maisha jela,” inasema hukumu hiyo.

Tukio lilivyofanyikia chooni
Kwa mujibu wa ushahidi uliopo katika mwenendo wa shauri hilo, siku ya tukio Julai 31, 2017 katika Shule ya Msingi Chomvu, mtoto huyo aliyekuwa mwafunzi wa darasa la tatu, alikwenda chooni kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo.

Wakati huo ilikuwa saa 5:00 asubuhi, mwalimu huyo (mshtakiwa) naye aliingia katika choo hicho hicho na kumshika mtoto huyo kisha kumziba mdomo kwa kutumia mkono ili asiweze kupiga kelele, ambazo zingesikika nje ya choo.

Hapo ndipo ndipo alipomvua mtoto huyo kaptula yake, kisha kumuingilia huku mtoto huyo akipata maumivu makali. “Nilitembea polepole kurudi nyumbani nikiwa na maumivu na nilikuwa natokwa na damu. Mshitakiwa aliniambia kama nitasema aliniingilia ataniua na kwamba niseme (damu) ilitokana na kuanguka,” sehemu ya ushahidi wa mtoto.

Source: Mwananchi
Mtu kama una hamu ya kufukua mtaro,.mbonamitandaoni mademu wanajitangaza wanatoa hivyo .Hela Yako tuu...Siyo unakwenda kutuharibia watoto wadogo kaah!
 
Asant majaji na hakimu wa mahakamani ya rufani na mwanzo Bado padir yule sostenez wapuuz Sana kuna nn kwemye makalio ambayo ss wengine hatujui
 
Maisha jela ni safi sana, nae aende kufanywa huko maisha...
 
Kuna tatizo mahali tena tatizo kubwa

Ova
 
Wangemnyonga tu kabisa. Tufiche wapi watoto jamani, wanaume tuoneeni huruma, tunazaa Kwa uchungu....hebu mdhibiti hizo nyege zenu.
Huu ni wakati wa mpito,na pia ushirikina unachangia,hivi mtu unashindwaje kushawishi mtu mzima hata kama hujui kushawishi sema mojamoja kwa moja naomba hiyo kitu nitalupia nitajie bei,kweli kabisa katika kumi wote watakataa
 
Kwahiyo walimu wa hisabati tumeshindwa kudhibiti nyege😳
 
Kuna tatizo mahali tena tatizo kubwa

Ova
Tatizo ni kubwa kuliko watu wanavyodhani mkuu.

Kama tusipofanya hatua za haraka, tunakwenda kuwa na kizazi cha ajabu sana.
 
Hilo tatizo mnalitizima katika angle gani?

Kwa namna tulivyosambaziwa maudhui ya aina hiyo kuanzia wasanii wetu na video zao na nyimbo zao... Connection za kila siku.. Sioni kama Kuna kupona

Kwa akili hii ya kibinadamu inayopenda soft and comfortable zone!? Sio ajabu kuona madume yakikazana kujaribu kupata ndogo na kutoa ndogo vile vile kutokana na upepo ulivyo Sasa.. Hao Celebrities na public figures ni uharo mtupu... Ndio role models wa vijana wetu..

Ni kama kizazi cha Kati hapo mabinti kujichubua Kwa kasi rangi ya ngozi.. Haikuwezekana kuwazuia.. Hadi madhara kuwa makubwa Sasa wametulia... Napo Dunia bado iko kasii.. Saiv wana fanya upasuaji kujirekebisha miundo ya miili Yao..

Tunajilisha upepo sana asee..!
 
Back
Top Bottom