Moshi: Mwenge wakwamisha mahabusu kupelekwa Mahakamani

Moshi: Mwenge wakwamisha mahabusu kupelekwa Mahakamani

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
Leo mahabusu wenye kesi mbalimbali kwenye mahakamani hasa Moshi Mjini, hawajafikishwa mahakamani kutokana na uhaba wa askari.

Askari wengi wapo kwenye shughuli ya uwashwaji wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa unaofanyika kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

Mgeni rasmi kwenye tukio Hilo ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Wengi wa mahabusu hao wapo gereza kuu la mkoa, Katanga na mpaka muda huu hakuna dalili za kufikishwa mahakamani.

Poleni sana mahabusu na ndugu mliofika mahakamani kuwaona jamaa zenu
 
Upungufu wa askari bado ni changamoto hope watapelekwa kesho na kuendelea
 
Back
Top Bottom