Moshi ndiyo wanaojua kusherekea Christmas na kuitendea haki

Moshi ndiyo wanaojua kusherekea Christmas na kuitendea haki

Artifact Collector

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
6,617
Reaction score
10,205
Kuna utofauti Mkubwa sana kulia Christmas Dar na Moshi

Tuanzie week ya maajilio ambao inaanzia jumapili ya mwisho ya November, ukiwa Dar makanisa hawana mda hata wa kuimba nyimbo za maajilio ni mwendo wa mapambio, vurugu vurugu, hakuna utaratibu. Mfano nyimbo karibu zote za Boney M. Kams First of Noel, Hark the Herald Angel sing, n.k zina swahili version, ukiwa Moshi ni kawaida kuimbwa kipindi cha maajilio Ila kwa Dar ni nadra sana.

Christmas Dar ni siku ya kawaida kama siku nyingine, yaani hakuna Ile feeling kwamba hii ni sikukuu. Ukiwa Moshi kuna feeling fulani unaiona kwamba sio siku ya kawaida huitaji kuambiwa.

Sherehe, ukienda Moshi Christmas kuna serehe kila baada ya nyumba kadhaa na mialiko kama yote, kitu ambacho Dar kila mtu kajifungia kwake na familia yake.

Christmas dar inaisha baada ya boxing day, Moshi kuanzia tarehe 20 mpaka 1 mwaka mpya ni Christmas party kweli kweli sio dar kuanzia tarehe 27 maisha yanaendelea kama kawaida.
 
Moshi kumenogaa
1671812115667.jpg
 
Back
Top Bottom