Moshi: RPC afafanua vielelezo vya wizi kuibwa Kituo cha Polisi na Askari Polisi kuchangishana kumlipa mwenye mali

Moshi: RPC afafanua vielelezo vya wizi kuibwa Kituo cha Polisi na Askari Polisi kuchangishana kumlipa mwenye mali

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Polisi wa Kituo Kidogo cha Polisi Uchira, Kata ya Kirua Vunjo Kusini, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro wanachangishana kumlipa shilingi 560,000 mkazi wa eneo hilo kabla ya Agosti 5 mwaka huu baada ya kuibwa vitu vyake vilivyokuwa ndani ya kituo hicho.

Vitu hivyo vilivyoibwa Julai 26, 2022 ni televisheni, pasi, kisimbuzi cha televisheni pamoja na nyaya za umeme ambavyo vilikamatwa na kuwekwa kituoni hapo kama vielelezo baada ya kuibwa.

"Maaskari wameniahidi kuwa kabla ya ljumaa watanilipa vitu vyangu, na kuwa kwa sasa hawana fedha, kwani mshahara wamemaliza, ila ninachotaka ni vitu vyangu na si kingine, kwa hivyo wanatumia njia mbadala kupata fedha" amesema mmiliki.

Diwani wa kata hiyo, Peter Meela amedai askari aliyekuwa zamu alitoka kidogo kwenda jengo la elimu karibu na kituo hicho cha polisi, ndipo mwizi aliingia kituoni na kuiba vitu hivyo vilivyokuwa vikishikiliwa.

Naye Kamanda wa Polisi mkoani humo, Simon Maigwa amesema huo ni wizi wa kawaida kama wanavyofanya wengine, na tayari mtuhumiwa amekamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

Source: Swahili Times


====================================

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amefafanua kilichotokea: "Ni kweli tukio hilo lilitokea, ilikuwa ni kesi ndogo na imetokea katika kituo kidogo cha Uchira ambacho kinafungwa saa 12 jioni.

"Mhusika ambaye aliiba ni mtuhumiwa ambaye tayari alishahukumiwa kifungo cha miezi miwili au faini, lakini kwa kuwa hakuwa na fedha ya kulipa akatumikia kifungo chake.

"Aliiba wakati kesi yake ikiwa inaendelea kwa kuwa alikuwa nje kwa dhamana, alifika kituoni hapo alfajiri na kuiba, alifanya hivyo ili kupoteza ushahidi wa kesi yake, hivyo utaratibu uliopo inamaanisha hapo ana kasi nyingine licha ya kuwa ni mfungwa.

"Kuhusu taarifa kuwa kuna askari wanachangishana ili kumlipa mwenye mali, hizo mimi sizijui, inawezekana ikawa kweli au si kweli, baada ya kuona taarifa hizo kwenye gazeti nilifungua faili kwa ajili ya upelelezi wa kufuatilia taarifa hizo.

"Ni jambpo dogo ambalo wengi wanalikuza, hivyo inawezekana kuna mambo yanaendelea na mimi sijajui ndio maana upelelezi unaendelea."
 
IMG-20220801-WA0028.jpg
 
Polisi wa Kituo Kidogo cha Polisi Uchira, Kata ya Kirua Vunjo Kusini, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro wanachangishana kumlipa shilingi 560,000 mkazi wa eneo hilo kabla ya Agosti 5 mwaka huu baada ya kuibwa vitu vyake vilivyokuwa ndani ya kituo hicho...
Mtuhumiwa keshakamatwa lakini vitu (ushahidi) havijakamatwa? kama vimekamatwa kwa nini wachangishane? kama havijakamatwa na tunajua kesi ni ushahidi huyo mtuhumiwa anashikiliwa kwa misingi ipi?
 
Polisi wa uchira bana anyway mirungi imewatajirisha sana walikua wanakula rushwa waz waz kama malaya mwiz wa shivaaz
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] iyo ndo moshi nayoijua mimi,
Mwizi anaiba kwenye kituo cha polisi, sasa sijui uko mtaani atakua anafanya nini[emoji119][emoji119]
 
Polisi wa Kituo Kidogo cha Polisi Uchira, Kata ya Kirua Vunjo Kusini, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro wanachangishana kumlipa shilingi 560,000 mkazi wa eneo hilo kabla ya Agosti 5 mwaka huu baada ya kuibwa vitu vyake vilivyokuwa ndani ya kituo hicho.

zi wa kawaida kama wanavyofanya wengine, na tayari mtuhumiwa amekamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.
Kwa hiyo mwizi kaiba mali alizoshtakiwa kuziiba 😀
 
Polisi wa Kituo Kidogo cha Polisi Uchira, Kata ya Kirua Vunjo Kusini, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro wanachangishana kumlipa shilingi 560,000 mkazi wa eneo hilo kabla ya Agosti 5 mwaka huu baada ya kuibwa vitu vyake vilivyokuwa ndani ya
Vitu vyote hivo ni laki tano tu
 
Halafu RPC anasema ni mambo madogo tuu ila watu wanayakuza!! Kuiba vielelezo tena kituoni kwake ni mambo madogo madogo? Serious? Hili ndo jeshi aliloliacha Sirro!!
 
Back
Top Bottom