Uchaguzi 2020 Moshi: Tundu Lissu ashindwa kuhutubia baada ya kuchelewa Mkutano wa Kampeni, aahidi kurudi

Hoja za kitoto saana maana "hujui kuwa hujui."

Kama wewe, na mashabiki wa huyo mropokaji, mlivyomkebehi Rais, alipoomba WaTz kufanya maombi, Mungu apishe mbali Korona, sasa mnakebehi nia yake njema ya kuombea Taifa limalize uchaguzi kwa amani. Kamwe nguvu za giza zitaweza kushinda nuru ya inayoangazwa kwa nguvu zake Mungu.
 
Nonsense [emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Na yule anayetaka asuguliwe na Sugu ananuaka damu za watanzania wangapi ?
 
Wapwa

Ni ukweli usiofichika kuwa CCM ina mbinu nyingi sana za uwizi wa kura, bahati mbaya nyingi tayari zimeshajulikana. Sasa kuna baadhi ambazo hazipigiwi kelele sana lakini ni mbinu mbaya sana na wakiitumia lazima watafaulu na kutakuwa hakuna pa kulalamika. mawakala muwe makini sana kwenye hili.

1 ) Watendaji kukusanya namba na vitambulisho vya kupigia kura
Kwa takribani miezi 6 sasa maeneo mengi sana, watendaji wamekuwa wakipita nyumba kwa nyumba kukusanya taarifa za wapiga kura, mfano namba ya kitambulisho na eneo unalopigia kura, kuna siku nliuliza hapa hizi taarifa wanazokusanya zinakwenda kufanyiwa nini hakuna aliyekuwa na jibu, na hii wamekuwa wakiifanya kwa siri sana.

Walichokipanga hawa jamaa, ni kwamba mfano kituo A kina wapiga kura 250, inajulikana ya kuwa sio wapiga kura wote watakaoenda kupiga kura, kwa hiyo mfano wakipiga kura watu 130, sababu tayari wana taarifa za wapiga kura wote wa kituo A wanaweza kujua nani amepiga nani hajapiga wakisaidiana na wasimamizi ndani ya kituo, kwa hiyo ni rahisi either kuleta mamluki kumalizia idadi iliyobakia wakiwa na taarifa sahihi za wapiga kura wa kituo husika au kutafuta upenyo wa kuongeza kura nyingine ndani ya box la kura. mfano wakiongoza kura 50 * vituo 50000 watakuwa wamefanikiwa kuongeza kura zaidi ya 2000,000+ .

Sasa nini kifanyike. Hapa tutagemea zaidi WAKALA kuhakikisha anajua idadi KAMILI ya watu wote waliopiga kura ndani ya kituo chake, na sio kupata idadi kutoka kwa msimamizi wa kituo. WAKALA hakikisha muda wote unakuwa kituoni, na kila anayeingia unamuhakiki sura yake ndani ya kitambulisho na unamuhesabu ili kutokuruhusu udanganyifu wowote wa idadi ya waliopiga kura.

2 ) Majimbo yaliyopita bila kupingwa

Haya majimbo yalikuwa ni mkakati wa kuongeza kura za uraisi kwao, huku kuna uwezekano mkubwa wa kupata 100% kwa kila kituo, kwa iyo tunaomba mawakala wetu muwe makini sana na wapiga kura na idadi ya watu watakaopiga kura ndani ya vituo vyenu.


Haki huinua Taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…