Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Wewe ni ujinga kweli kama makonda. Kwani wanaoishi Moshi ni wachaga pekee? Ukiambiwa waumini waliokufa ni makabila nje ya Kilimanjaro utashangaa?
Bwege sana wewe!
Tangu lini akasikia mchaga anaitwa Mwamposa. Je angeitwa tena Nabii Mrema nadhani angeomba atolewe ngozi
 
Wiki iliyo pita nilikutana na mzee mmoja ivi barabaran akanipa kijikaratasi ( kipeperushi) kidogo kikidhungumzia hili kongamano la huyu anaejiita nabii mwamposi dah baada tu ya kusoma kilichoandikwa kwenye kile kijikaratasi nilisikitika sana sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hali inatosha sana hivi sasa
 
uchunguzi ufanyike na hatua za kisheria zichukuliwe haraka kwa viongozi hao wa dini kwa kusababisha maafa kwa watanzania wenzetu,
pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna pale matembele ya pili, napo kitalia mda si mrefu. Tusubiri mwaka unasifuri nyingi huu.
 
Kwanini akamatwe? Hakuwa na vibali? Ameshatoa maelezo take polisi na kwasasa yupo uraiani.
Hapo kwa haraka haraka kuna makosa matatu makubwa yaliyo wazi kabisa (japo mimi siyo mtaalamu wa fani za makosa ya jinai).

La kwanza ni utapeli. Kuwaaminisha watu mambo ya uongo na yasiyokuwa na ushahidi wa kisayansi.

Kosa la pili ni kuhatarisha maisha ya watu. Kuwaitisha watu wengi kama mtego ili wagombanie kitu alichowaaminisha kuwa ni cha thamani. Hapa madhara ni watu kukanyagana.

La tatu ni kusababisha vifo (manslaughter). Mtu akifanya kitu chochote kisha kile kitu kikasababisha kupoteza maisha hapo atakuwa na kosa la manslaughter. (Mnielimishe zaidi hapa, maana sina taaluma sahihi kwenye hili).

Conclusion yangu ni kuwa akamatwe haraka kisha huduma yake isimamishwe haraka kupisha uchunguzi wa kina.

Ikiwezekana iundwe tume ya wataalam wayamulike makanisa kuona usalama wa huduma za haya makanisa.

Hayo yataepusha tusije tukafika walikofika mapadre wazungu waliokuwa wanawafira watoto na vijana wa seminar miaka nenda rudi bila kuwajibishwa.

Asante
 
Tapeli sana huyo dogo, ni mwenyeji wa Chunya-Mbeya, mlevi wa kupindukia Leo anadanganya tu watu kujifanya ni nabii
 
Makosa yake yapo wazi kabisa. La kwanza ni utapeli na la pili ni kuhatarisha maisha ya watu. La tatu ni kusababisha vifo (manslaughter).
Mkuu Hapo huwezi kujastify utapeli kwani hili ni swala la imani. Kumbuka makusanyiko yake yote yanakuwa na idadi kubwa ya watu na yanavibali vyote vinavyohitajika. Kwenye situation Kama hi huwezi kum- sue mtu isipokuwa tunaita tu ni bahati mbaya. Hapo walioathirika ndio wajinga.
 
Shetani ana mbinu nyingi za kumtumia Mwanadamu ili kuthihirisha ufalme wake.
Alimtumia mzee moja wa huko Arusha akawa anatoa kikombe cha dawa ya miti maarufu kama kikombe cha Babu. Huyu naye alikuwa anatumia jina la Yesu. Sasa hivi huyu babu hatumskii tena.
Wako manabii wengi sana wa uongo hapa Tanzania ambao wanatumia Jina la Yesu Kristo.
Yesu Kikristo alisema " watakuja manabii wengi wa uongo na watatoa pepo kwa jina langu"
Ukiona muhubiri anakuwa na Kanisa lake, Mhasibu wa Sadaka ni yeye na mtunza fedha ni mke wake au binti yake ujue hiyo si kutangaza ne no la Mungu ila ni Biashara.
Kwa kifupi Ufalme wa shetani haudumu kamwe na wafuasi wake nao hawadumu kamwe,
Tujiepushe na Manabii wa Uongo.
Serikali izuie Taasisi za Dini za watu Binafsi ambazo hazina mfumo wa Kikanisa na zinakusanya sadaka na kuzitumia kwa maslahi binafsi bila kulipa kodi.
 
Mkuu labda utuambie wewe hili tukio unalionaje, kwamba ni tukio la kawaida tu na watu hawatakiwi kusema kitu?
Kwahiyo kama halijawahi kutokea tena, basi tusiongee tukae kimya?
Wewe huoni kama kuna uzembe uliofanyika kwa upande wa waandaaji (akiwepo mchungaji) uliopelekea watu 20 kufa?
Na je unachukuliaje kitendo cha mchungaji kuondoka zake baada ya watu 20 kufariki as if nothing happened, akaishia airport?
 
wale wakristo mnisaidiye kuna mahala kwenye biblia yesu aliwapaka mafuta watu,kuuza vitambaa,maji,chumvi na kupokea bahasha zenye pesa?je pia alipofanya miujiza alijitangaza?
 
Wameangamia kwa kukosa maarifa. Mafuta ya upako yana tofauti gani na irizi za waganga wa kienyeji?
Ifike mahali serikali ilinde raia wake dhidi ya utapeli wa kidini.
Yote haya ni watnzania kukosa matumaini kwenye maisha hivyo kuweka imani kwenye mambo ya ajabu ajabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…