Nsumba ntale tz
JF-Expert Member
- Apr 19, 2016
- 713
- 762
Waumini 18 wa Dini ya Kikristo wamefariki dunia usiku huu mjini Moshi, wakati wakikanyagana kugombea kukanyaga mafuta ya upako katika kongamano la kidini la Mtume Boniface Mwamposa, DC wa Moshi Kippi Warioba amethibitisha
Updates: 00:45
Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa kukanyagana imefikia 20 na uenda idadi hiyo ikaongezeka Mkuu wilaya amethibitisha.
UPDATES:
Watu 20 wamefariki dunia leo jioni Jumamosi Februari 1,2020 katika ibada ya mahuburi wakati wa harakati za kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' katika Viwanja vya Majengo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Inadaiwa kuwa waumini hao walikumbwa na maafa hayo wakati wakikanyagana kwa ajili ya kugombania kukanyaga mafuta yaliyomwagwa na mhubiri huyo yakidaiwa kuwa na upako.
Inaelezwa kuwa watu zaidi ya 40 walikanyagana katika harakati za kugombania mafuta ya upako na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.
Idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka kwa kuwa hakuna taarifa ya ujumla ya majeruhi waliopelekwa katika vituo vya afya vya jirani pamoja na Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amelithibitisha leo saa 5:00 usiku kuwa taarifa za awali waumini 20 wamekufa lakini akasisitiza hizo ni taarifa za awali.
“Taarifa za awali tulizonazo ni kuwa ni waumini 20 wamepoteza maisha lakini tunaendelea kufuatilia maeneo mengine ya zahanati, vituo vya afya na hospitali kama kuna watu walipelekwa huko,” amesema Kippi.
Apostle Boniface Mwamposa a.k.a Bulldozer
=====
MWAMPOSA ATAKIWA POLISI KWA MAHOJIANO
Jeshi la Polisi limemtaka Boniface Mwamposa kujisalimisha polisi kwa mahojiano ya vifo vya watu 20 vilivyotokea mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro usiku Februari Mosi, 2020
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Elia Mwambapa ndiye aliyeomba kibali cha kongamano hilo la siku tatu lililomalizika jana Jumamosi
Amesema baada ya hilo tukio wamemtafuta sana huyo Boniface Mwamposa maarufu kama Bulldozer bila mafanikio. Na kumtaka ajisalimishe kwa mahojiano
Kamanda Hamduni alifafanua kuwa idadi ya waliokufa ni 20 hadi sasa, ambapo kati yao watoto wadogo ni wanne, watu wazima 16
11:24 AM: MWAMPOSA AENDESHA IBADA KANISANI KWAKE KAWE
Wakati Polisi wakidai kumtafuta bila mafanikio, Mwamposa yupo anaendesha ibada kanisani kwake Kawe jijini Dar huku kukiwa na ulinzi mkali
Inadaiwa watu wanadhibitiwa kupiga picha bila kibali na ibada ya leo itaisha saa 6 kamili mchana
ATOA TAMKO KUHUSU VIFO MOSHI
"Sijafanya mauaji, bali nilikuwa katika kutangaza na kuponya kupitia ufalme wa Mungu. Hakuna kafara pale bali muda wao uliisha na wameitwa na Bwana Yesu watakakoishi milele.
Najiandaa niende nikajisalimishe Polisi Moshi. Bwana ametoa na bwana ametwaa" Mch. Mwamposa
12:47 PM: ATIWA MBARONI
Jeshi la Polisi jijini Dar limemtia mbaroni Mwamposa (almaarufu Bulldozer) kufuatia vifo vya watu 20 na majeruhi 16 huko Moshi, Kilimanjaro
Mwamposa aliwaaga waumini wake mchana huu kuwa anaenda Moshi kuitikia wito wa Polisi
WALIOFARIKI MOSHI KUAGWA KWA PAMOJA KESHO
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Anna Mghwira amesema miili ya watu 20 waliofariki dunia kwa kukanyagana kwenye ibada wakigombea kukanyaga ‘mafuta ya upako’ itaagwa kesho kwenye uwanja wa Majengo, Moshi. Tayari miili 16 imeshatambuliwa.