Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Mkuu mtaji wa wajinga huu hakuna reasoning kabisa
Daah hatua za haraka lazima zi chukuliwe kulinda wananchi na wimbi hili la manabii hewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hatua lazima zichukuliwe kwa dharura. Haya makanisa yaundiwe chombo maalum cha kuyaangalia usalama wa hizo huduma wanazotoa. Tusije tukafikia yale ya mapadre wazungu waliokuwa wanawafira watoto wadogo makanisani na mashuleni.
 
Waumini 18 wa Dini ya Kikristo wamefariki dunia usiku huu mjini Moshi, wakati wakikanyagana kugombea kukanyaga mafuta ya upako katika kongamano la kidini la Mtume Boniface Mwamposa, DC wa Moshi Kippi Warioba amethibitisha

Updates: 00:45
Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa kukanyagana imefikia 20 na uenda idadi hiyo ikaongezeka Mkuu wilaya amethibitisha.

UPDATES:
Watu 20 wamefariki dunia leo jioni Jumamosi Februari 1,2020 katika ibada ya mahuburi wakati wa harakati za kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' katika Viwanja vya Majengo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Inadaiwa kuwa waumini hao walikumbwa na maafa hayo wakati wakikanyagana kwa ajili ya kugombania kukanyaga mafuta yaliyomwagwa na mhubiri huyo yakidaiwa kuwa na upako.

Inaelezwa kuwa watu zaidi ya 40 walikanyagana katika harakati za kugombania mafuta ya upako na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.

Idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka kwa kuwa hakuna taarifa ya ujumla ya majeruhi waliopelekwa katika vituo vya afya vya jirani pamoja na Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amelithibitisha leo saa 5:00 usiku kuwa taarifa za awali waumini 20 wamekufa lakini akasisitiza hizo ni taarifa za awali.
“Taarifa za awali tulizonazo ni kuwa ni waumini 20 wamepoteza maisha lakini tunaendelea kufuatilia maeneo mengine ya zahanati, vituo vya afya na hospitali kama kuna watu walipelekwa huko,” amesema Kippi.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Mhubiri huyo alielekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akitaka kuondoka, lakini ndege aliyokuwa amepangwa kuondoka nayo ilichelewa (delayed) na ndipo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro lilipomtia mbaroni uwanjani hapo.
Apostle Boniface Mwamposa a.k.a Bulldozer

Chanzo: Mwananchi
Tatizo ni viatu wanavyovaaga walokole ni vile 4 angles 'foengo' vyenye visigino vya mbao asa inategemea ukanyagwe usoni afu uwe fresh tu . kingine unakuta mgonjwa kachomolewa hospitali hali taabani afu umpeleke akaombewe then katka hali yake hyohyo ya ugonjwa akagombee mafuta si akisukumwa mara moja tu ashakufa???
 
Nilicho gundua watu walio wengi humu Jf mnapenda kuongelea vitu kimihemko sana na porojo za kuchangamsha akili kuliko kuongelea uhalisia ambao una ukweli wa kutosha ambao haupendwi wala kusikilizwa na watu wengi wajinga,
Mara nyingi Mwamposa amekuwa akiandaa makongamano ya kukanyaga mafuta Dsm na watu wengi kuponywa na kokote aliko enda halijawahi tokea tatizo lolote iweje Moshi wakati wa kukanyaga mafuta bahati mbaya wengi wakadondoka na kukanyagana, mtu anatokea aliko toka eti "wajinga ndio waliwao" mnamkosea sana Mungu,
Jifunzeni kufanya research vya kutosha kabla ya kutenda wala kuongea lolote, kuna mtu ame-reply eti mafuta ya upako ni kama hirizi tu, na yametajwa hadi kwenye biblia na matumizi yake, Muogopeni Mungu,
PUM..VU.

Kwa hiyo umejiona umetoa point za maana kwa sisi unaotuita tunapenda porojo.Uliyoandika yote ni ovyo,rudia kusoma ulichiandika halafu jisikilize namna ulivyoandika pumba tu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
Mathayo 7:15

Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
Mathayo 24:24

kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule.
Marko 13:22

Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.
2 Petro 2:1

Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
1 Yohana 4:1
 
ni kweli kifo hakizoeleki ndugu lakini kuwalaumu wahanga na kumuunganisha mhubiri kabla ya ripoti ya uchunguzi toka kwenye mamlaja husika tunakosea au tuseme tunaongozwa na hisia.

mashariki ya kati kila mwaka idadi kadhaa ya mahujaji hukutwa na visa hivyo hivyo wakiwa kwenye zoezi la kurusha mawe kwenye mnara na imeshapokelewa na kuzoeleka; watu na mamlaka za huko hazichukui tahadhari kubadili utaratibu.

kwa mlinganyo huo, kuna tofauti gani na hilo?

FaizaFoxy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
@I am Bless: Usiseme kwamba watu wengi wanakurupuka bali jiulize na fanya kuushirikisha vyema ubongo wako.

Iweje mahosptilani wagonjwa ni wengi na kama hawa wanaojiita manabii wanauwezo wa kutibu kwa nini watu waende hospitali badala ya kwenda kwenye haya makanisa?.

Kwa nini watu wahangaike kufanya kazi ilihali wakienda kwa hao mitume wanafanikiwa kupata mkate na kuendeleza familia zao?

Kwa nini watu wahangaike na matatizo ambayo wakipakwa mafuta au maji hayakomi ila inakuwa ni utumwa wa kila leo unataka upate mafuta hayo au maji hayo?

Kwa nini hamtaki kukubali ukweli kwamba hawa sio manabii wa ukweli wameweka mbele maslahi ya wao kuwa na miujiza ambayo ukiifikiria kwa undani zaidi haieleweki?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi naona ukifikiria kwa undani zaidi siyo kwamba haieleweki. Inaeleweka sana tu kwamba hao ni matapeli kabisa wanaotumia matatizo na kukosa maarifa kwa watu kujinufaisha.
 
Waumini 18 wa Dini ya Kikristo wamefariki dunia usiku huu mjini Moshi, wakati wakikanyagana kugombea kukanyaga mafuta ya upako katika kongamano la kidini la Mtume Boniface Mwamposa, DC wa Moshi Kippi Warioba amethibitisha

Updates: 00:45
Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa kukanyagana imefikia 20 na uenda idadi hiyo ikaongezeka Mkuu wilaya amethibitisha.

UPDATES:
Watu 20 wamefariki dunia leo jioni Jumamosi Februari 1,2020 katika ibada ya mahuburi wakati wa harakati za kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' katika Viwanja vya Majengo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Inadaiwa kuwa waumini hao walikumbwa na maafa hayo wakati wakikanyagana kwa ajili ya kugombania kukanyaga mafuta yaliyomwagwa na mhubiri huyo yakidaiwa kuwa na upako.

Inaelezwa kuwa watu zaidi ya 40 walikanyagana katika harakati za kugombania mafuta ya upako na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.

Idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka kwa kuwa hakuna taarifa ya ujumla ya majeruhi waliopelekwa katika vituo vya afya vya jirani pamoja na Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amelithibitisha leo saa 5:00 usiku kuwa taarifa za awali waumini 20 wamekufa lakini akasisitiza hizo ni taarifa za awali.
“Taarifa za awali tulizonazo ni kuwa ni waumini 20 wamepoteza maisha lakini tunaendelea kufuatilia maeneo mengine ya zahanati, vituo vya afya na hospitali kama kuna watu walipelekwa huko,” amesema Kippi.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Mhubiri huyo alielekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akitaka kuondoka, lakini ndege aliyokuwa amepangwa kuondoka nayo ilichelewa (delayed) na ndipo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro lilipomtia mbaroni uwanjani hapo.
Apostle Boniface Mwamposa a.k.a Bulldozer

Chanzo: Mwananchi
MWAMPOSA APIGWE BAN KUFANYA MIKUTANO YAKE YA KITAPELI ,Ona amesababisha MAAFA.
 
Wapumzike kwa amani, niko njiani kuelekea msibani kuna mwenzetu kakanyagiwa huko!
 
Nilicho gundua watu walio wengi humu Jf mnapenda kuongelea vitu kimihemko sana na porojo za kuchangamsha akili kuliko kuongelea uhalisia ambao una ukweli wa kutosha ambao haupendwi wala kusikilizwa na watu wengi wajinga,
Mara nyingi Mwamposa amekuwa akiandaa makongamano ya kukanyaga mafuta Dsm na watu wengi kuponywa na kokote aliko enda halijawahi tokea tatizo lolote iweje Moshi wakati wa kukanyaga mafuta bahati mbaya wengi wakadondoka na kukanyagana, mtu anatokea aliko toka eti "wajinga ndio waliwao" mnamkosea sana Mungu,
Jifunzeni kufanya research vya kutosha kabla ya kutenda wala kuongea lolote, kuna mtu ame-reply eti mafuta ya upako ni kama hirizi tu, na yametajwa hadi kwenye biblia na matumizi yake, Muogopeni Mungu,
Kiwango chako cha kufikiri kiko chini ya kijivu. Kamwone mtaalam au msomi yoyote akusaidie.
 
Hili tukio lingetokea usukumani hili.......sipat picha
 
Back
Top Bottom