Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Hata uchagani wapo kumbe wajinga? Mbona huwa mnasema humu kuwa wachaga wamesoma sana? Au hawakuelimika? Pole zao!
Kwani umeambiwa hao marehemu 20 ni Wachaga? Unaamini kila aliye Dar es Salaam ni Mzaramo, na kila aliyeko Chato au Kolomije au Serikalini ni Msukuma?
 
Yaani kiongozi wa dini upande wa kikristo anaweza kufanya chochote kwa waumini na wakatii...Poleni sana
 
Huyo mwamposa afunguliwe kesi ya uhujumu uchumi ili asipate dhamana kabisa. Watu 20 ni wengi kuwatoa kafara kwa mara/mkupuo mmoja. Uongo uongo wake na hayo mafuta yake ya gizagiza akanyage yeye.
 
Kusiwe na Double Standard,Kitendo alichokifanya Mwamposa si cha kiungwana hata kidogo,waamini wake 20 wamekufa yeye amepanda ndege na kurudi Dar kwenda kawe kuhubiri,Huyo jamaa anastahili kifungo,kwanza inabidi awekwe ndani kwa usalama wake maana sie tunaamini ametoa kafara ndio maana haijamgusa kabisa,kwa usalama wake tunaomba polisi mumuuhifadhi ndani kwa mda mpaka uchungu wa kuondokewa na ndugu zetu 20 upungue.

Here we go again, unaleta tena ramli chonganishi eti " Mwamposa akamatwe na kufunguliwa mashitaka" unataka ashitakiwe kwa kosa lipi hasa?

Vifo vimesababishwa watu kukanyagana, kila mtu alitaka kuwahi kukanyaga mafuta hawakutaka kufuata utaratibu walio wekewa na wahudumu - hapo ungetegemea nini kama sio maafa?

Haya mambo ya kumlahumu Mwamposa kwamba aliondoka bila ya kutoa msaada wowote - tuhuma hizo hazina ukweli wowote kwani wahudumu wake ndio wahusika wakuu wa kuongoza wahumini kukanyaga mafuta.

Kwa taarifa yako Mwamposa alazimiki kuwepo masaa yote wakati wahumini wanakanyaga mafuta, binafsi nina uhakika kwamba wakati wa stampede Mwamposa alikuwa amekwisha ondoka uwanjani.

Hapa naona mnaleta mwendelezo wenu wa kampeini za kumpiga vita Mwamposa, kinacho endelea hapa nyinyi mnakuwa driven by wivu mkishirikiana na washindani wake ambao waliwahi kupendekeza kwa JPM eti "akina Mwamposa na WRM awafunge na kupiga marufuku dini zao!"
 
Dini.
Endeleeni kuamini huyo jamaa yenu toka juu atashuka tu kudadeki. Tukiitwa nyani tunapiga kelele ila the majority wana-act ka monkeys.
 
Yaani kiongozi wa dini upande wa kikristo anaweza kufanya chochote kwa waumini na wakatii...Poleni sana
Siyo dini ya Kikristo tu. Hata dini nyingine, wajinga wa dini wapo kila sehemu. Hao wajinga wa dini wanakuwa wepesi kuwa-brainwashed na kufanywa religious extremists kisha wanaanza kupelekeshwa kama mbwa wa mwindaji. Hata magaidi wengi ni religious idiots wanaokuwa brainwashed na wanadanganywa na baadae kuamrishwa kufanya ujinga kwa kisingizio cha kuitetea imani/dini yao. Kwa maneno mengine hata hao wanaodanganywa na kuamini eti wakikanyaga mafuta wataondokana na shida walizonazo hadi kufikia hatua ya kuuana kwa kukanyagana hawana tofauti na gaidi anayeaminishwa kwamba akijilipua na kuua wengine atakwenda mbinguni! Wote ni wajinga wa dini.
 
Waumini 18 wa Dini ya Kikristo wamefariki dunia usiku huu mjini Moshi, wakati wakikanyagana kugombea kukanyaga mafuta ya upako katika kongamano la kidini la Mtume Boniface Mwamposa, DC wa Moshi Kippi Warioba amethibitisha

Updates: 00:45
Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa kukanyagana imefikia 20 na uenda idadi hiyo ikaongezeka Mkuu wilaya amethibitisha.

UPDATES:
Watu 20 wamefariki dunia leo jioni Jumamosi Februari 1,2020 katika ibada ya mahuburi wakati wa harakati za kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' katika Viwanja vya Majengo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Inadaiwa kuwa waumini hao walikumbwa na maafa hayo wakati wakikanyagana kwa ajili ya kugombania kukanyaga mafuta yaliyomwagwa na mhubiri huyo yakidaiwa kuwa na upako.

Inaelezwa kuwa watu zaidi ya 40 walikanyagana katika harakati za kugombania mafuta ya upako na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.

Idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka kwa kuwa hakuna taarifa ya ujumla ya majeruhi waliopelekwa katika vituo vya afya vya jirani pamoja na Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amelithibitisha leo saa 5:00 usiku kuwa taarifa za awali waumini 20 wamekufa lakini akasisitiza hizo ni taarifa za awali.
“Taarifa za awali tulizonazo ni kuwa ni waumini 20 wamepoteza maisha lakini tunaendelea kufuatilia maeneo mengine ya zahanati, vituo vya afya na hospitali kama kuna watu walipelekwa huko,” amesema Kippi.
Apostle Boniface Mwamposa a.k.a Bulldozer

=====

MWAMPOSA ATAKIWA POLISI KWA MAHOJIANO

Jeshi la Polisi limemtaka Boniface Mwamposa kujisalimisha polisi kwa mahojiano ya vifo vya watu 20 vilivyotokea mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro usiku Februari Mosi, 2020

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Elia Mwambapa ndiye aliyeomba kibali cha kongamano hilo la siku tatu lililomalizika jana Jumamosi

Amesema baada ya hilo tukio wamemtafuta sana huyo Boniface Mwamposa maarufu kama Bulldozer bila mafanikio. Na kumtaka ajisalimishe kwa mahojiano

Kamanda Hamduni alifafanua kuwa idadi ya waliokufa ni 20 hadi sasa, ambapo kati yao watoto wadogo ni wanne, watu wazima 16
jamaaa limetoa bonge la kafara aise hapo lazima mafanikio yaonekane ...
 
Hata uchagani wapo kumbe wajinga? Mbona huwa mnasema humu kuwa wachaga wamesoma sana? Au hawakuelimika? Pole zao!
[/QUOTE
Mbona maka watu 5000 walikufa kwa kukanyagana nao je??hiyo ni ajali tu acheni kulopoka
 
Here we go again, unaleta tena ramli chonganishi eti " Mwamposa akamatwe na kufunguliwa mashitaka" unataka ashitakiwe kwa kosa lipi hasa?

Vifo vimesababishwa watu kukanyagana, kila mtu alitaka kuwahi kukanyaga mafuta hawakutaka kufuata utaratibu walio wekewa na wahudumu - hapo ungetegemea nini kama sio maafa?

Haya mambo ya kumlahumu Mwamposa kwamba aliondoka bila ya kutoa msaada wowote - tuhuma hizo hazina ukweli wowote kwani wahudumu wake ndio wahusika wakuu wa kuongoza wahumini kukanyaga mafuta.

Kwa taarifa yako Mwamposa alazimiki kuwepo masaa yote wakati wahumini wanakanyaga mafuta, binafsi nina uhakika kwamba wakati wa stampede Mwamposa alikuwa amekwisha ondoka uwanjani.

Hapa naona mnaleta mwendelezo wenu wa kampeini za kumpiga vita Mwamposa, kinacho endelea hapa nyinyi mnakuwa driven by wivu mkishirikiana na washindani wake ambao waliwahi kupendekeza kwa JPM eti "akina Mwamposa na WRM awafunge na kupiga marufuku dini zao!"
Usizunguke. Hii mwamposa tayari katoa kafara maisha ya watu wasio na hatia, tena mwanzoni kabisa mwa mwaka. Kwani ndiyo mara yake ya kwanza kuwakanyagisha watu hayo matunguli yake?
 
Dini.
Endeleeni kuamini huyo jamaa yenu toka juu atashuka tu kudadeki. Tukiitwa nyani tunapiga kelele ila the majority wana-act ka monkeys.
Kwani dini ndiyo zinafanya watu kuwa manyani? Au huu unyani wetu unataka kutupia lawama kwenye dini?
 
Jamani, kwanini aliweka mafuta machache mpaka watu wakanyagane hivo, hakukua na utaratibu wowote ile kukanyaga kwa zamu labda duh, hii inaonesha jinsi watu tuko desperate, matatizo, kiasi ukiambiwa chochote unafata tu so sad.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mimi sijawahi kwenda kwenye ibada zake lakini naambiwa wakati wa kukanyaga mafuta watu huwa wanateleza na kuanguka kwahio hata kama mafuta yangewekwa mengi bado hili lingetokea
Watu wakiwa wengi alafu kila mtu anataka awe wa kwanza kukanyaga lazima wakajagane I feel sorry kwa hao watoto wadogo waliokufa kwasababu ya wazazi wao
So sad
 
Pamoja na Mungu kuendelea kuwaumbua hawa manabii wa uongo lakin mijitu imeendelea kuzba macho na maskio yao. Alianza kumuumbua Mzee wa upako,akaja Gwajima na sasa Mwamposa. Chaajabu wiki ijayo ukienda kanisani utakuta mijitu bado imejaa ikisubiri kununua mafuta ya upako.

Sjui Mungu atumie mbinu gani kutuonyesha kuwa hawa ni manabii wa uongo?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mungu mwenyewe kashajichokea ameamua kuwaacha tu
Maana huwaambii kitu ni kama wapo dunia nyingine 🤦🏽‍♀️
 
Usizunguke. Hii mwamposa tayari katoa kafara maisha ya watu wasio na hatia, tena mwanzoni kabisa mwa mwaka. Kwani ndiyo mara yake ya kwanza kuwakanyagisha watu hayo matunguli yake?

Reading between the line unaonekana wazi wazi una chuki binafsi, he/she goes "Mwamposa katoa kafara maisha ya watu wasio na hatia, tena mwanzoni mwa mwaka" unarudia ngojera za waganga wa kienyeji wanao practice RAMLI CHONGANISHI, FYI Mwamposa ni mkristo - kama unafikiri Mwamposa ni mfuga majini no body will take you seriously save your like mind.
 
Mbona hamsemi hizi ni njama za serikali kuzima sakata la makonda? Hahahaaaaaaa 😆😆😆
 
Duh babu... Haya Ni Mambo ya kiimani.. hayafanywi kwa mpangilio huo unaouongelea...

Na nashauri mnapochangia nyuzi za kiimani Kama hizi, msiconclude as if nyie Sasa ndiyo mnaojua wa kweli yupi na asiye wa kweli yupi.

Sasa mtu unachangia mada Kama hizi kwa fujo, hata hujawahi kuhudhuria ukaona watu wamedanganyika na lipi, au hukuweza kuridhishwa na lipi.

Mnaoponda huduma anazotoa ambazo habagui imani ya watu, Ni kuwakosea Watanzania wengi wengine wanaonufaika na huduma zake..

Mamia kwa mamia ya matasa, wasiokuwa na ajira, wasiokuwa na mitaji, wenye biashara zisizofanikiwa, wenye viwanja walioshindwa kujenga, wenye kudai bila mafanikio, wenye kudai madeni yasiyolipika, mabubu, viziwi, viwete, waliopooza, magonjwa ya moyo, Figo, walioondolewa kizazi na kupoteza fikra za kupata watoto, na shida nyingine mbalimbali,Watanzania wenzetu wametatuliwa...

Asidharauliwe mtu anayeenda tafadhali. Nilipata kunywa chai kwa mama lishe mmoja wa imani nyingine,yeye alisema mdogo wake kwa miaka 7 alikuwa hajapata mtoto, akaenda Kawe, Sasa kupata mtoto na akamwambia mumewe kuwa huyu mtoto Nampa jina la Boniface. Sasa utawaonaje wajinga watu wa Aina hiyo.

Tusivuke mipaka. Makongamano yake hufikia watu elfu 5 hivi nadhani, au hata Mara mbili yake..! Sasa wote hao sio wajinga, au njaa Kama baadhi ya wachangiaji humu wanavyodhani. Babu la Bara,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Sijafanya mauaji, bali nilikuwa katika kutangaza na kuponya kupitia ufalme wa Mungu. Hakuna kafara pale bali muda wao uliisha na wameitwa na Bwana Yesu watakakoishi milele.

Najiandaa niende nikajisalimishe Polisi Moshi. Bwana ametoa na bwana ametwaa" Mch. Mwamposa
 
Back
Top Bottom