Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Waziri wa mambo ya ndani amethibitisha kuwa nabii mwamposya yuko ndani ya mikono ya jeshi la polisi yeye na wenzake.

Mwamposya anaweza kuendelea kushikiliwa mpaka pale itapobainika kuwa hana kosa la kujibu

Leo asubuhi mwamposya aliwaaga waumini wake kanisani kwake katika viwanja vya kanisa lake maeneo ya tanganyika pekazi Dar es salaam na kuelekea mkoani Kilimanjaro analikotakiwa kujisalimisha.

USSR

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Pamoja na Mungu kuendelea kuwaumbua hawa manabii wa uongo lakin mijitu imeendelea kuzba macho na maskio yao. Alianza kumuumbua Mzee wa upako,akaja Gwajima na sasa Mwamposa. Chaajabu wiki ijayo ukienda kanisani utakuta mijitu bado imejaa ikisubiri kununua mafuta ya upako.

Sjui Mungu atumie mbinu gani kutuonyesha kuwa hawa ni manabii wa uongo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Adhabu ya muuaji ni kuuawa na yeye

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Subiri Vyombo vya dola vifanye kazi yake,kibali mwisho ilikuwa saa 18:00 yeye aliendelea hadi usiku.

Vyombo vya dola vinaongozwa na watu wenye busara na weledi, hawawi driven na misplaced emotions na chuki binafsi.

Mara ngapi tumewahi kushuhudia mamia ya mashabeki wa mpira wakipoteza maisha kutokana na stampede - wapi uliwahi kusikia wamiliki wa klabu,makocha na wamiliki wa viwanja wakifikishwa Mahakamani kutokana na maafa ya mashabeki kukanyagana na kufa?

Mtasema sana na mengine mnaongeza chumvi tu just to demonise Mwamposa kutokana na chuki binafsi na wivu wa kitoto, kumbukeni amewasaidia watu wengi wenye shida zilizo shindikana - kama mnafikiri maelfu ya watu ambao u-attend kongomano zake ni mapunguani ie hawana akili na nyinyi mnajiona ni above average Joe, basi endeleeni kuamini hivyo lakini sio kumtakia binadamu mwenzako mabaya.
 
Reading between the line unaonekana wazi wazi una chuki binafsi, he/she goes "Mwamposa katoa kafara maisha ya watu wasio na hatia, tena mwanzoni mwa mwaka" unarudia ngojera za waganga wa kienyeji wanao practice RAMLI CHONGANISHI, FYI Mwamposa ni mkristo - kama unafikiri Mwamposa ni mfuga majini no body will take you seriously save your like mind.
Kuwa mkristo siyo hoja ya mashiko. Hata baadhi ya malaika waligeuka kuwa shetani, sembuse mkristo tu!! Vijikanisa vyote vinavyoendekeza kujifanya vinatoa tumiujiza ujiza ni vijikanisa uchwara na vingi vinatumia nguvu za giza ili kujipatia ufahari hapa dunia badala ya kuwaambia watu ukweli.

Yesu mwenyewe kama binadamu alipitia mateso na giriba za dunia. Baadhi ya watu awataki shida, akipatwa na changamoto kidogo anachanganyikiwa mwisho anaangukia mikononi mwa matapeli wanaotumia vijikanisa kuwadanganya hadi wanakanyagana wapate kukanyaga matunguli ya mganga "mwamposa".

Mimi sina chuki na mwamposa. Nisichopenda ni vijikanisa vya kijasiliamali vinavyowadanganya watu na kuwapumbaza hadi kuwaibia hata kidogo walichopatiwa na Mungu kama riziki ya kuendesha maisha yao wanawapelekea hao manabii fake. Sasa wameenda mbali na kuwatoa kafara!!
 
Bukyanagandi,
Hakuna busara sehemu ambayo umevunja sheria maana hakuna aliye juu ya sheria. Nchi inaongozwa na katiba na sheria/kanuni. Kama ukivunja sheria haingalii busara au kwamba huyu ni mchungaji.
 
Unatuzungumzia watanzania kwan sisi hatuna midomo, 87.99% ya watanzania tunaamini hio ni kafara
Reading between the line unaonekana wazi wazi una chuki binafsi, he/she goes "Mwamposa katoa kafara maisha ya watu wasio na hatia, tena mwanzoni mwa mwaka" unarudia ngojera za waganga wa kienyeji wanao practice RAMLI CHONGANISHI, FYI Mwamposa ni mkristo - kama unafikiri Mwamposa ni mfuga majini no body will take you seriously save your like mind.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anajua anachokizungumza huyu devil worshipper
"Sijafanya mauaji, bali nilikuwa katika kutangaza na kuponya kupitia ufalme wa Mungu. Hakuna kafara pale bali muda wao uliisha na wameitwa na Bwana Yesu watakakoishi milele.

Najiandaa niende nikajisalimishe Polisi Moshi. Bwana ametoa na bwana ametwaa" Mch. Mwamposa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom