LESIRIAMU
JF-Expert Member
- Feb 12, 2008
- 9,006
- 14,536
MOSHI: WAZIRI SIMBACHAWENE AMELIONYA JESHI LA POLISI KUBAMBIKIZA WATU KESI.
#Moshi: Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amelionya Jeshi la Polisi kwa tabia za baadhi ya askari wake kubambika watu kesi, huku pia akitaka mafunzo ya awali ya askari yaongezwe kutoka miezi tisa hadi 12 ili kupunguza changomoto ya ukosefu wa maadili kwa baadhi ya askari.
Akizungumza jana Julai 23 na wakufunzi pamoja na wanafunzi wa shule ya polisi Tanzania (TPS), Simbachawene amesema kumekuwepo na manung'uniko makubwa dhidi ya jeshi la polisi kutoka kwa raia ikiwemo watu kubambikiwa kesi, jambo linaloleta taharuki kwenye jamii.
"Kuna manung'uniko makubwa dhidi ya Jeshi la polisi ,kuna kuonea watu kesi za kubambikiza, hata kwenye uaadilifu katika kumkamata mtu kwa mujibu wa sheria unakuta mtu ambaye hana nia ya kukufanyia fujo wewe unataka kumletea ukamanda wako, sio kila mahali ni vita,"amesema Simbachawene
Amewataka kujitahidi kuwa waadilifu na kujiepusha na tabia za ulevi
“Jambo ambalo linawaangusha huko mtaani mnakoishi ni tabia zenu ikiwemo pia na ulevi. Ngao mlizovaa ni kwenda kumwakilisha Rais kwenye maeneo mnayosimamia lakini unakuta ni mlevi na mnafanya maamuzi ya ovyo mkifanya hivyo hamtafika mbali."
"Kidogo tunachangamoto katika uadilifu ,wakati mwingine kazi ya polisi inataka kuonekana kama ni kazi ya watu ambao hawamjui Mungu ,kumbakiziza kesi mwenzako wewe ni sawa na muuaji, katika changamoto kubwa katika maisha ni kuuguliwa na kesi kufa sio tatizo," amesema Simbachawene
Kuhusu mafunzo, amesema: “Kuna haja ya kuwekeza katika shule hii ili iweze kutoa mafunzo mazuri ,na nafikiria hata training (mafunzo) yetu ya askari wapya ya miezi tisa naona ni ndogo tufanye miezi 12 watu wapate mafunzo ya kueleweka," amesema Simbachawene
Amesema Wizara hiyo ina kazi kubwa ya kuhakikisha inaandaa askari wenye uadillifu na waliofundishwa vizuri maadili ya kazi.
Sasa IGP tii maagizo ya waziri