Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 11,129
- 7,321
Nilichosikia mimi kwa safari hii kilichowaponza Israel ni matumkzi yao ya Digital Technology, kwamba kwa sasa wanayo mitambo inayoona kila kitu kinachoendelea kwenye uande wa mahasimu waoMwaka 1973 Israeli ilishambuliwa na Misri na Syria kwa kushtukizwa wakati wa majira ya sikukuu ya Yom Kippur. Misri walivuka mfereji wa Suez na kuingia Israel(Sinai). Wasyria nao wakaingia huko Golan.
Hali ilikuwa tete sana kwa Israel hadi jeshi likaamua kuwa liwaache Wasyria wafanye wanavyotaka wao wadeal na mwenye nguvu, Misri.
Ukiisoma ile vita, habari za kijasusi kuhusu vita kutoka Mossad na MI ziliwafikia wakubwa mapema. Lakini siasa zilifanya wawe wazito kuchukua maamuzi.
Kwenye Movie Golda(2023), Waziri mkuu wa wakati huo, Golda Meir anasikika akisema kuwa kumobilize jeshi wakati wa sikukuu za Yom Kippur ni kutaka kujiua kisiasa na kuwapa wapinzani cha kusema.
Kwenye demokrasia, maamuzi makubwa, hata yanayohusu usalama wa nchi hutanguliza kwanza maslahi ya kisiasa kisha ya nchi ndiyo yanafuata.
Idara za ujasusi za Israeli zilishutumiwa vikali sana baada ya vita ya Yom Kippur, lakini ni ngumu sana idara hizi kufanya kazi zake vizuri kwenye mazingira ya kidemokrasia.
Jana tena, kwenye msimu wa Yom Kippur, asubuhi ya sabato Israel imeshambuliwa na Hamas kwa style ile ile ya 1973. Miaka 50 ya kumbukumbu ya vitw ya Yom Kippur!!. Tena imeshambuliwa baada ya kutokea machafuko makubwa ya kugombania "siasa" ndani ya Israeli.
Si rahisi kwa chombo kama Mossad kutofahamu kuhusu shambulio lililotokea jana. Lakini ni wanasiasa ndiyo wanaofanyia kazi taarifa za kijasusi. Na wanasiasa wanafanya maamuzi kwa kutanguliza maslahi ya kisiasa mbele.
Maoni yangu: Siasa za kidemokrasia ni hatari kwa usalama wa nchi. Zinaweza kukwamisha hata kazi za taasisi bora kama Mossad.
Kumbe maadui hawa walikuwa wameshawagundua Israel kwamba wanatumia teknoloji, halafu wao wakaamua kutumia FOOT AND MOUTH" classical teknoloji. Nasikia dakika za mwisho kuna mtu aliwa-alert Israel kuwa HAMAS walikuwa wanapanga sahmbulio, lakini Israel wali-ignore baada ya mitambo yao kuwaonyesha taarifa tofauti.