Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Watu watano wanaripotiwa kutiwa mbaroni katika nchi za Tanzania, Ghana na Senegal wakihusishwa na jaribio lililotibuliwa la shambulio dhidi ya Watalii wa Israel, Kituo cha Televisheni cha Channel 12 cha Israel kimeripoti.
Kituo hicho kimenukuu taarifa za kiintelijensia zikionesha kuwa watu hao waliokamatwa walipata mafunzo ya Wapiganaji wa Quds wenye mafungamano na Jeshi la Iran (Islamic Revolutionary Guards Corps), ikiongeza kuwa kukamatwa kwao kumetokana na taarifa za Majasusi wa “Magharibi.”
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Watano hao walipewa mafunzo na vifaa, ambayo havikubainishwa, kutoka Lebanon na kutumwa katika mataifa hayo ya Afrika chini ya mwamvuli wa kuwa Wanafunzi wa Kidini, wakiwa na ‘misheni’ ya kuwatafuta watalii wa Kiyahudi na kuwashambulia.
Ripoti hiyo imetaja Shirika la Upelelezi la Israel (Mossad) kuhusika na kutibua mpango huo, bila kubainisha hasa kuhusika kwake ni kwa namna gani. Hakuna uthibitisho uliotolewa kutoka mataifa yote yaliyohusika (Israel, Iran na nchi za Afrika). Iran imekana kuhusika, ikisema madai hayo hayana msingi wowote.
Watu wote hao wamekamatwa kabla hawajafanikiwa kutekeleza azma yao, kwa mujibu wa ripoti, bila kubainisha hasa mahali walipokamatwa, huku ikitaja kuwa washambuliaji hao wanaendelea kufanyiwa mahojiano.
Chanzo: Times of Israel