The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Katibu wa Chama cha Makandarasi Wanawake Kanda ya Kusini, Mossi Mzee Nampembe, amejitokeza rasmi kuwania nafasi ya udiwani wa viti maalum kupitia Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) katika Kata ya Nachingwea, Wilaya ya Lindi mkoani Lindi.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu, Mossi, ambaye pia ni msanifu barabara, alieleza kuwa uamuzi wake unalenga kutumia maarifa yake yote kuwahudumia wanawake na jamii kwa ujumla ndani ya Manispaa ya Lindi.
Mossi ameongeza kuwa anaamini uzoefu wake katika sekta ya ujenzi na maendeleo ya jamii utakuwa chachu ya mabadiliko chanya kwa wanawake na vijana wa Nachingwea, akitoa wito kwa wanawake wengine kujiamini na kushiriki kikamilifu kwenye siasa na uongozi.