Most expensive schools in Tanzania

Kuna watu wanatoka mapovu mazito apa.....umaskini ni ugonjwa sure
 
Umasikini ni mbaya sana
Maana kila kitu unaona ni gharama,

Mtoto anayesoma Feza International
Akifika anapewa vitabu vyote, madaftari kila yakiisha, kalamu anapewa, nguo anafuliwa
Shuka anapewa
Darasani wanasoma wachache sana na kila somo unahama darasa na kwenda darasa la somo husika
Wana ECA ya arts, music, cooking (girls only) IT
Mwalimu anapewa wanafunzi wake anawafatilia, mwalimu anatembelea nyumbani kwa mtoto kuongea na wazazi

Kuna mengi sana hufanywa na hizi international School na ndio maana watu wanalipa 10000+ dollars ili mwanae awe pale

Lazima tukubali kua Kuna shule zinaandaa rulers na zingine the ruled
 
Watakuwepo vipi Top ten wakati hawatumii mitaala ya Tanzania I mean NECTA. wenyewe ni IB and IGCSE curriculums...
Yaani hawa hawajui cha mtemi Mkwawa, Mirambo, Majebele au Makwaia, hakuna cha Afro Shirazi Party wala TANU, hizo historia zenu hazipo kwenye Mitaala yao, ukimpeleka pale kuanzia chekechea ni kwamba anatayarishwa kusoma majuu, yeye atajuwa kizazi cha Queen Elizabeth II zaidi kuliko vita yenu ya Maji Maji..
Sawa kabisa watu hawajaelewa hizi shule mtoto anafundishwa kwa lengo gani...
 
Hakuna shule nazoziamini kama za VETA, yaani mtoto akishatoa ujinga tu na Form 4, akikubali kwenda VETA basi nina uhakika mtoto hatakufa njaa, ni shule ya kufundisha maarifa na ujuzi, umesema la maana sana mkuu..Ningeshukuru wazazi wengi wangelifikiria hili...
 
Mimi ikitokea mtu anataka nimsaidie kumsomesha, nitakuwa tayari kumsomesha veta tu
 

Wazazi wengi bado ni watumwa wa elimu ya vyeti badala ya maarifa......na hii ni kutokana muundo wa soko letu la ajira na ndio maana ajira ndio zinalalamikiwa kuwa na ujira mdogo sana.......

Dunia imebadilika lakini wazazi wengi bado wana fikra mgando......

Sasa hivi ajira hakuna muandae kijana wako ajiajiri kwa kupata maarifa sahihi na sio idadi ya vyeti......
 
Nadhani pia mtaala unakuwa updated kila mwaka kuendana na current worlwide trends za kisiasa,biashara,teknolojia na uchumi.

Tofauti na sie wa kayumba tuliofundishwa mambo ya pendulum bob na mpaka wanafunzi wa mwaka 2090 watasoma hayo hayo. Leo hii ukizungumzia hybrid technology kwenye physics hamna mtu anaejua zaidi ya wale wanafunzi wafuatiliaji wa habari za dunia ambazo hazipo kwenye syllabus
 
Kabisa kabisa, na akitoka pale anaweza ku-top up elimu yake vyuo vya ufundi mpaka kumalizia kwenye vyuo vyetu vikubwa..
Anawiva kimaarifa, kiufundi na kiujuzi..na hapo ni kwa mtoto wa kike au wa kiume, no limitations..
Pia anaweza chagua baada ya internship, aajiriwe au ajiajiri, safi kabisa..
 
Kaka mie nilikua naenda pale kucheza mpira km watu toka nje timu iliitwa cabs ,kn vitu nikajifunza nimekuja kuviona miaka ya karibuni ,wale wako updated kila siku
 
Kaka mie nilikua naenda pale kucheza mpira km watu toka nje timu iliitwa cabs ,kn vitu nikajifunza nimekuja kuviona miaka ya karibuni ,wale wako updated kila siku
Dah ina maanisha wale wanafundishwa michongo ya maana inayotokea mamtoni huko. Sie tunasoma mambo ya kina chief mkwawa hadi leo hii. Jauuuu sana yani mie necta naonaga ya kipuuzi sana kukomoana tu.
 
Utumwa wa kiakili ndio huu, yani kulipa kwa dollar wewe ndio unaona ufahari?
 
Dah ina maanisha wale wanafundishwa michongo ya maana inayotokea mamtoni huko. Sie tunasoma mambo ya kina chief mkwawa hadi leo hii. Jauuuu sana yani mie necta naonaga ya kipuuzi sana kukomoana tu.
Mkuu ulishapeleka mtoto hizi medium english school?sasa kule kuna maujanja mara 1000,mfn climate change nilijua miaka ya 99_2000,we tumeisikia 2010,[emoji23] ,tuishia hapa tufanye kazi
Nb cjasoma ist,ila nimekua pale kucheza mpira kn niliyojifunza
 
Mkuu, mtoto aliyesoma IST unataka afikirie kufua?,sijui kupika?.Hayo ni mawazo ya uku uswahilini.
Hahahaha nimecheka kwa sauti mkuu! Ila kweli mambo ya kujua kuosha vyombo na nini ni akili zetu waswazi kwa kuwa housegel kwetu ni anasa wakati kwao ni kazi kama kazi nyingine. Na ndiyo maana mtu haoni aibu kusema hajui kufua coz washing machines zipo [emoji23][emoji23]
 
Hata wewe hutakubali kuona motto wako aliyekuwa na malezi bora karudi likizo nyumbani na kiingereza kizuri ila ni teja.
Una maana hawa mateja wote hapa nchini ni product ya hizo shule ....!!!!???
Ikiwa ni hivyo basi watz wengi ni matajiri kwa kuwapeleka watoto huko kwenye kujifunza uteja .Tupunguze chuki na kujibidiisha ,tunaweza kufanikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…