SoC03 Motisha katika kuweka lengo kuwa hai

SoC03 Motisha katika kuweka lengo kuwa hai

Stories of Change - 2023 Competition

Petro Masunga

Member
Joined
May 5, 2023
Posts
7
Reaction score
7
Haya ndiyo maisha haijalishi ni mambo gani unapitia, lakini fanya jambo moja kuwa hai, kwamba haya ndiyo maisha.

Nimewaza sehemu niliyopo sasa, na pia nikafikiria niliko toka, nikashika tama, ama kweli haya ndiyo maisha.

Ni mambo mangapi nilitamani huko nyuma, sikuweza kupata? Nilidhani kwamba kama ningepata hayo yote niliyokuwa natamani, hakika maisha yangu yatakuwa bora zaidi na ya kuvutia.

Muda wa hayo ulipofika, sijaona kama maisha yangu yamekuwa bora hata kidogo, maana furaha siyo ile ambayo nilitarajia, na maisha siyo yale ambayo nilitarajia. Hivyo huwezi kuyafanya maisha yako kuwa bora, bali uko na uwezo wa kufanya vitu bora zaidi na vya kupendeza katika maisha, lakini maisha yatabaki kama maisha.

Hivyo pale ulipo hayo ndiyo maisha ya binadamu, na mwisho wa yote hayo ni udhalimu, maana mwenye mwili hatapata chochote pale. Lakini jambo lililo bora zaidi ni furaha, hutapata furaha baada ya kufariki, bali furaha utaipata kwa sababu unaishi, yaani uko hai ndiyo furaha.

Haijalishi hayo maisha yanakupeleka wapi, lakini kwa sababu uko hai hii ndiyo furaha. Furaha siyo kwa sababu unapata vitu, bali furaha ni kwa sababu unafanya vitu katika hayo maisha. Hii ndiyo furaha ya kuwa hai.

Hili ndilo jambo bora zaidi na la kupendeza nililoliona katika siku za kuwa hai katika maisha haya, na huu ndiyo motisha wangu kwako.

Asante!
 
Upvote 2
Back
Top Bottom