Motivation stories/Kusoma vitabu vya biashara ni kazi bure tu kama hujakaina hari ulio nayo kwa sasa.

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Now day kuna motivations stories nyingi sana, Uki google utakutana na stories za kila aina,

Kuna hadi Motivation speaker wakina James Mwang'amba na wengineo kila siku utawasikia wapo Holday inn wanatoa stories za matumaini

Kuna vitabu vya kutosha kabisa na kuna watu wanavisoma kila siku.

Kuna story kwenye mitandao ya kijamii jinsi mtu alivyo anza na my be sh elfu 10 na sasa ni tajiri au jinsi alivyo fuga na sasa yuko mbali.

Ni kwamba Hizi story ni kazi bure kama wewe hujajikana.

Vitendo kama vya Uchangudoa, Ushoga, kutumia madawa ya kulevya, Ulevi na kadhalika huwa hawa watu wanaacha kabisa hivi vitendo.

Ili changudoa aamue kuacha Uchangudoa lazima aukane huo Uchangudoa kutoka moyoni mwake.

Shoga anaweza acha ushoga pale tu atakapo chukia ushoga kutoka moyoni mwake.

Changudoa bila kuukana Uchangudoa anaweza jikuta ameolewa na bado akaendelea kujiuza kwa sababu hakuwahi kuukana uchangudoa.


Kuamua kuwa mjasiriamali lazima uukane umasikini, lazima uuchukie umasikini na lazima uchukie kutumikishwa na lazima haya yatoke moyoni mwako.

Bila kuukana na kuchukia utumwa utaishia kujaza Flash disk na story za walio fanikiwa na usifanye chochote.

Utasoma kila aina ya vitabu na utajaza vitabu nyumbani kwako ila hutafanya chochote.

Hii ni kwa sababu hujawahi ikana hari ulio nayo kwa sasa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha kukatisha watu tamaa

Wengi tu wanafanikiwa na wako inspired kwa kusoma na kupitia vitabu mbalimbali

Mimi tu nimejianzisha biashara na inaenda vizuri baada ya kusikiliza speech za waliofanikiwa katika ujasiliamali

Ukishindwa wewe ni wewe na sababu zako huko, tafadhali pambana na hali yako!
 
Kabisa yani,

Watu wamefanya MOTIVATIONs kuwa kama FASHION...yani mtu akisikia story tu basi na yy anataka afanye bila kudhamiria moyoni na akilini, mwisho wa siku anakuwa wa kushika shika vitu vingi5 bila kuvimaliza.

Ukiuchukia umaskini na kutumikishwa utakua mjasiriamali/mfanyabiashara mzuri sana.
 
Andika vizuri hiyo heading..... mtu mzima hovyooo

Sukari Yenu
 
Rudia kusoma nilicho andika nazani umeanza na Comment. sasa rudi ukasome kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna nilipo sema ukisoma vitabu huwezi fanikiwa, shida zenu huwa mnakurupuka ku coment bila kusoma. huna tofauti na wale walio saini mikataba ya madini wao walisaini bila kusoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kabisa,poor people have poor habit

great thinker
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…