OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Ni kwa muda mrefu wafanyakazi wamekuwa wakiambiwa wanafanya kazi za kitumwa. Mawazo kama haya yako tangu zamani sana.
Wakati wa vita baridi kati ya Usoshalisti na Ubepari, nchi nyingi za Afrika zilisema hazina upande lakini baadae wakaelemea kwenye Usoshalisti, taifa kama Tanzania likaweka kitu chake kilichoitwa ‘ujamaa’
Ili kufanya wafanyakazi wawachukie mabosi wao, Ujamaa ukasema kuwa matajiri ni wanyonyaji wa wafanyakazi, wafanya biashara ni wanyonyaji wa wakulima. Kwa sera zilizoshindwa kuangalia mazingira halisi.
Watu wakaiamini serikali na kwenda serikalini, na wengine kuacha kuwauzia wafanyabiashara wakubwa. Matokeo yake wakaanza kulalama maslahi madogo, yaani wakaona walipokuwa wanaambiwa wananyonywa kulikuwa na maslahi kuliko huku ambapo waliambiwa kuko vizuri.
Kwa sababu hiyo kukawa na migomo ya kimya kimya, ambayo ilitekelezeka kwa uvivu makazini hali iliyopelekea shughuli za serikali kuzorota. Kwenye biashara, raia wakaanza kupeleka biashara zao nje, ili kupata maslahi maana serikali ilikuwa inanunua kwa bei ya chini sisiyo ridhisha. Hapo biashara za magendo zikapanda chati.
Kwa sasa wameibuka vijana waliojiajiri kuongea, motivational speakers, ambao kiuhalisia wanapita mulemule ambapo Sera za Ujamaa zilipita na kusababisha majanga. Wafanyakazi wanaaminishwa kuwa wananyonywa na wengine wanaoamini huacha kazi na kujikuta katika hali mbaya zaidi mitaani.
Mifano wanayotumia kuwaonyesha watu waliofanikiwa haizingatii sheria za kitakwimu bali huamua kuwataja wachache waliofanikiwa ambao pia huwa hawaangalii sababu nyingine za kufanikiwa kwao.
Sikatai kwamba ni vizuri mtu kuwa na biashara zake lakini, kutumia 100% ya hela uliyojisevia ya mashahara kwenye biashara ni kujiua kwa kuwa biashara ina vitu vingi hujitokeza katikati.
Kwa kuwa biashara inataka kuongezewa hela mara kwa mara, kunakuwa na haja ya kuwa na chanzo cha mapato ili kuifinance biashara yako ambayo inaweza kuwa mikopo au mshahara unaoupata kwenye kazi yako.
Wapo wengi wanabiashara kubwa lakini pia bado wameajiriwa na wanapata mapato zaidi ya sehemu moja.
Kwa wafanyakazi wote, ni vyema kusoma zaidi masuala ya kibiashara na sio kufuata ushauri wa motivational speaker ambaye hajui kitu kuhusu biashara yasije kutokea kama yanayowakuta wengine.
Signed
OEDIPUS