Ramthods
JF-Expert Member
- Jun 2, 2009
- 515
- 187
Motivational speakers wanawaambia watu kitu ambacho watu wanapenda kusikia. Wanafahamu kuwa watu wengi wanapenda kujiajiri, hivyo na wao wanaingia na gia hiyo hiyo.
Ukweli ni kwamba, sio kila mtu anaweza kujiajiri. Kujiajiri sio jambo la uamuzi tu, bali ni jambo ambalo linategemea uwezo wako pia. Kwa watu wengine kuajiriwa ni uamuzi mzuri zaidi. Wapo watu walioajiriwa na wamefanikiwa katika maisha. Ingawa ni wachache, lakini hiyo inaonyesha kufanikiwa katika ajira ni kitu kinachowezekana, na wewe unaweza kuwa mmoja kati ya hao wachache.
Ushauri wa motivational speakers ni ushauri wa "jumla". Ushauri mzuri ni ushauri ambao ni "personal". Badala ya kuwafuata motivational speakers, ni bora kuwa na "personal coach/adviser" mtu ambae atakupa ushauri kwa kuzingatia mazingira yako, uwezo wako, vipaji vyako etc.