Motivational speaking

Motivational speaking

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Umeshawahi kujiuliza kwanini chizi haumwi anapokula vitu vichafu lakini mwenye akili huwa anaumwa anapokula vitu vichafu? Je unadhani ni kipi kinachomfanya mgonjwa wa akili asiumwe wakati yeye ana mwili kama wako na ana tumbo kama lako? Kitaalamu mtu anapokuwa ana tatizo la akili, yaani hana akili vizuri kuna baadhi ya hofu huwa zinaondoka kwenye akili yake.

Huwa hafikirii matokeo ya alichofanya, ila huwa anafanya anachoona sawa kufanya kwa wakati huo anaofanya. Chizi au mgonjwa wa akili huwa haumwi kwa sababu hana hofu ndani ya moyo wake, ndio maana hapati madhara kama anayopata mtu timamu anapofanya kitu cha madhara. Hofu ndio adui mkubwa na anaweza kukutengenezea maradhi hata sehemu ambayo haina maradhi.

Licha ya kuwa dunia inapitia kwenye changamoto ya maradhi hatari ya Corona,
lakini hofu pia inachangia idadi ya vifo kuongezeka. Sikwambii usichukue tahadhari hapana, chukuwa tahadhari ila ondoa hofu. Hofu ndio inayokufanya ushindwe kufanikiwa miaka yote kwa sababu unaamini kuwa chochote utakachokifanya hakiwezi kuwa.

Hofu inakufanya kila siku kuzalisha migogoro kwenye ndoa yako, kwa sababu umempenda mtu ambaye humuamini, hivyo unahofu naye. Siku utakayoondoa hofu akilini mwako, utastaajabu namna milango ya fursa itakavyofunguka.

Jifunze kutoka kwenye matatizo ya wengine lakini usihofu kutenda eti kwa sababu wengine walianguka walipotenda. Hofu inaweza kumuua mgonjwa kitandani hata kama vipimo vinaonesha hana tatizo. Ondoa hofu ili ufanikiwe kwa sababu wenye hofu huwa hawafanikiwi.
 
Kuna kina mama wawili hapa wanachambana toka saa 1 asubuhi hadi sasa hivi.Ama kweli wazaramo wanajua kuongea.
 
Tangu lini Nyumbu wakamtakia mema rais Samia hadi wampangie cha kufanya?

Hangaikeni na mzee wa MIGA mtetezi wa mashoga.
 
KUNA KINA MAMA WAWILI HAPA WANACHAMBANA TOKA SAA 1 ASUBUHI HADI SASA HIVI.AMA KWELI WAZARAMO WANAJUA KUONGEA.
Wapi hapo nije kuchukua habari, me ni reporter wa tandahima FM ya mmkakonde...
 
Jifunze kutoka kwenye matatizo ya wengine lakini usihofu kutenda eti kwa sababu wengine walianguka walipotenda. Hofu inaweza kumuua mgonjwa kitandani hata kama vipimo vinaonesha hana tatizo. Ondoa hofu ili ufanikiwe kwa sababu wenye hofu huwa hawafanikiwi.
 
Hofu inakufanya kila siku kuzalisha migogoro kwenye ndoa yako, kwa sababu umempenda mtu ambaye humuamini, hivyo unahofu naye. Siku utakayoondoa hofu akilini mwako, utastaajabu namna milango ya fursa itakavyofunguka.
 
Hofu ndio inayokufanya ushindwe kufanikiwa miaka yote kwa sababu unaamini kuwa chochote utakachokifanya hakiwezi kuwa.
 
Nje ya mada, baada ya kusoma hili bandiko nimemkumbuka kichaa mmoja alikuwa anakatiza Mikumi kwa miguu mara kibao tu Simba walichokuja kumfanya siri yake na Simba wale.
 
Ilikuwaje...! Walimfuturu!?
 
Umeshawahi kujiuliza kwanini chizi haumwi anapokula vitu vichafu lakini mwenye akili huwa anaumwa anapokula vitu vichafu? Je unadhani ni kipi kinachomfanya mgonjwa wa akili asiumwe wakati yeye ana mwili kama wako na ana tumbo kama lako? Kitaalamu mtu anapokuwa ana tatizo la akili, yaani hana akili vizuri kuna baadhi ya hofu huwa zinaondoka kwenye akili yake.

Huwa hafikirii matokeo ya alichofanya, ila huwa anafanya anachoona sawa kufanya kwa wakati huo anaofanya. Chizi au mgonjwa wa akili huwa haumwi kwa sababu hana hofu ndani ya moyo wake, ndio maana hapati madhara kama anayopata mtu timamu anapofanya kitu cha madhara. Hofu ndio adui mkubwa na anaweza kukutengenezea maradhi hata sehemu ambayo haina maradhi.

Licha ya kuwa dunia inapitia kwenye changamoto ya maradhi hatari ya Corona,
lakini hofu pia inachangia idadi ya vifo kuongezeka. Sikwambii usichukue tahadhari hapana, chukuwa tahadhari ila ondoa hofu. Hofu ndio inayokufanya ushindwe kufanikiwa miaka yote kwa sababu unaamini kuwa chochote utakachokifanya hakiwezi kuwa.

Hofu inakufanya kila siku kuzalisha migogoro kwenye ndoa yako, kwa sababu umempenda mtu ambaye humuamini, hivyo unahofu naye. Siku utakayoondoa hofu akilini mwako, utastaajabu namna milango ya fursa itakavyofunguka.

Jifunze kutoka kwenye matatizo ya wengine lakini usihofu kutenda eti kwa sababu wengine walianguka walipotenda. Hofu inaweza kumuua mgonjwa kitandani hata kama vipimo vinaonesha hana tatizo. Ondoa hofu ili ufanikiwe kwa sababu wenye hofu huwa hawafanikiwi.
Asante Mshana Jr.

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom