Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Umeshawahi kujiuliza kwanini chizi haumwi anapokula vitu vichafu lakini mwenye akili huwa anaumwa anapokula vitu vichafu? Je unadhani ni kipi kinachomfanya mgonjwa wa akili asiumwe wakati yeye ana mwili kama wako na ana tumbo kama lako? Kitaalamu mtu anapokuwa ana tatizo la akili, yaani hana akili vizuri kuna baadhi ya hofu huwa zinaondoka kwenye akili yake.
Huwa hafikirii matokeo ya alichofanya, ila huwa anafanya anachoona sawa kufanya kwa wakati huo anaofanya. Chizi au mgonjwa wa akili huwa haumwi kwa sababu hana hofu ndani ya moyo wake, ndio maana hapati madhara kama anayopata mtu timamu anapofanya kitu cha madhara. Hofu ndio adui mkubwa na anaweza kukutengenezea maradhi hata sehemu ambayo haina maradhi.
Licha ya kuwa dunia inapitia kwenye changamoto ya maradhi hatari ya Corona,
lakini hofu pia inachangia idadi ya vifo kuongezeka. Sikwambii usichukue tahadhari hapana, chukuwa tahadhari ila ondoa hofu. Hofu ndio inayokufanya ushindwe kufanikiwa miaka yote kwa sababu unaamini kuwa chochote utakachokifanya hakiwezi kuwa.
Hofu inakufanya kila siku kuzalisha migogoro kwenye ndoa yako, kwa sababu umempenda mtu ambaye humuamini, hivyo unahofu naye. Siku utakayoondoa hofu akilini mwako, utastaajabu namna milango ya fursa itakavyofunguka.
Jifunze kutoka kwenye matatizo ya wengine lakini usihofu kutenda eti kwa sababu wengine walianguka walipotenda. Hofu inaweza kumuua mgonjwa kitandani hata kama vipimo vinaonesha hana tatizo. Ondoa hofu ili ufanikiwe kwa sababu wenye hofu huwa hawafanikiwi.