Tetesi: Moto wa Rais Magufuli watua NHC

Tetesi: Moto wa Rais Magufuli watua NHC

Dindilimunyo

Senior Member
Joined
Sep 12, 2016
Posts
108
Reaction score
206
Taarifa za kunyapia nyapia zinasema mambo ndani ya Shirika la NHC sio shwari. Pamoja na JPM kuonekana ana mahaba na Mchechu na anafurahishwa na kazi yake mambo inasemekana sio shwari kwa baadhi ya vigogo ambao inasemekana wamemkabidhi Mkurugenzi barua za kuacha kazi.

Taarifa zinasema hali hiyo ya vigogo kuacha kazi inatokana na Mchechu kuwa mkali kupita kiasi kwa sasa. Inasemekana amewapiga chini kwenye vitengo nyeti baadhi ya wakurugenzi kwenye shirika hilo na kupangua pangua majukumu hali ambayo wengi wao hawaridhiki nayo.

Hali kadharika kuna vigogo wa shirika hilo wamekuwa wakihojiwa na vyombo vya dola kuhusika na tuhuma mbali mbali za ufisadi kwenye shirika hilo jambo hilo nalo linachochea kuacha kazi kwa vigogo hao mmoja wao inasemekana kashahamia NMB. Kubwa linalowakimbiza vigogo hao ni tuhuma mbali mbali zinazowakabili hasa ufisadi wa miradi mbali mbali ya shirika hilo.

Moja ya mradi unao onekana kuwa kaa la moto ni ujenzi wa Jengo lao la makao makuu ambalo insemekana ujenzi umegharim B19 na ukarabati wake yani Fnshng umelamba B15. Inasemekana vigogo hao wamekuwa wakihojiwa mara kwa mara na Takukuru juu ya sakata hilo na sasa watapandishwa kizimbani wakati wowote.

Soon nitawatajia vigogo hao stay tune
 
Mkuu kasema wanajifukuza wenyewe kwa matendo yao1
 
Bwaga manyanga...uliweka ugoko nikaweka jiwe sasa unaumia mwenyewe.
Embe lilokwiva hujiangua mtini tayari kwa kuliwa...mwenye kung'amua hana haja ya kuuliza hapa
 
Mbona wadaiwa wengine hawakutolewa vitu nje?ujinga tu na chuki za kipuuzi
 
hakuna kuleana tena watu wamepiga sana haya mashirika
 
Samaki mwenye magamba hawezi kujizika na kuishi miongo kwenye matope ni kambale tu baada ya kukosa maji
 
Taasisi ya NHC lazima tuichunguze kwani Kuna zigo wamelibeba la madeni makubwa ya kibenki muda wowote watamwachia mnyamwezi.
 
Back
Top Bottom