Moto waunguza Bweni la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mbeya University of Science and Technology - MUST)

Moto waunguza Bweni la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mbeya University of Science and Technology - MUST)

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Taarifa ni kuwa kuna bweni la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mbeya University of Science and Technology) linaungua kwa moto leo Mei 20, 2025.

UPDATES... ( Taarifa ya Mtandao wa Mustso_updates)
Moto mkubwa ulizuka katika Hostel za Wasichana 8C lakini umekwisha kudhibitiwa, mpaka sasa hakuna aliyejeruhiwa lakini taratibu zingine za kiusalama zinaendelea kuchukuliwa ikiwemo kuwahamisha wakazi wote wa jengo hilo kwenda Hostel mpya. Aidha tunapenda kutoa salamu za pole kwa wahanga wote wa janga hili tunawaweka kwenye maombi ili afya zao zirejee vyema.

TAARIFA YA CHUO
Akizungumza na JamiiForums.com, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya Prof. Aloys Mvuma amesema "Moto haujateketeza jengo, ni chumba kimoja cha bweni ndicho kilichokuwa kinaungua, hakuna mtu ambaye amejeruhiwa zaidi ya mali kadhaa, tathimini kamili ya athara iliyojitokeza bado haijajulikana.

"Chanzo pia cha moto hakijajulikana lakini moto huo uliotokea asubuhi ulifanikiwa kudhibitiwa na wenzetu wa Zimamoto."
WhatsApp Image 2025-05-20 at 12.42.37_2d28167b.jpg
 
Nchi imeingia kwenye ombwe tayari, maana leo kila upande wa nchi unataarifa zilizo changamka...
Ebu ngoja tusubiri kusikia hayati atasema nini...🙄
 
moto ni miongoni mwa ajali zinazoweza wakati wowote.

ni vizuri kua wastahimilivu na wenye subra wakati vyombo husika vya kudhibiti majanga vikiendelea na kazi yao ya uokozi na kudhibiti janga hilo baya, na hatimae uchunguzi maalumu utabainisha chanzo cha janga hilo 🐒
 
GrTNxQpXcAAV_TH.jpeg
 
Back
Top Bottom